MBWANA Samatta, mshambuliaji wa timu ya Aston Villa alitumia dakika 65 ndani ya Uwanja kuonyesha makeke yake mbele ya Leicester City wakati timu yake ikishinda mabao 2-1.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni nusu fainali ya Kombe la Carabao ulichezwa kwenye uwanja wa Villa Park, ambao ulikuwa wa marudio baada ya ule wa kwanza timu zote kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa nyota huyu Mtanzania ambaye alitolewa dakika ya 66 alianza kikosi cha kwanza jumla na alikosa nafasi mbili ambazo leo akizitazama atazijutia kwa kushindwa kupachika mabao hayo huku moja alilofunga dakika ya 37 alikuwa ameotea na nafasi yake ikachukuliwa na Davis alipotolewa.
Kocha Mkuu wa Aston Villa, Dean Smith alishuhudia uwezo mkubwa wa mlinda mlango wake Orjan Nyland aliyeokoa michomo mingi ya hatari huku Mtanzania Samatta naye akionyesha uwezo wake kwenye mechi yake ya kwanza ndani ya Aston Villa iliyompa kandarasi ya miaka minne na nusu.
Mabao ya Aston Villa iliyotumia mfumo wa 3-4-3 yalifungwa na Matt Target dk 12 na lile la ushindi likifungwa na Trezeguet dk ya 90+3 lililowachanganya Leicester ambao walifunga bao dk ya 72 kupitia Kwa Iheanacho. Ushindi huo unaipeleka Aston Villa hatua ya fainali na watacheza na mshindi wa leo kati ya Manchester City na Manchester United, Uwanja wa Wembeley.
0 COMMENTS:
Post a Comment