January 29, 2020


JONAS Mkude, kiungo wa Simba ambaye amedumu kwa muda mrefu amesema kuwa leo ndani ya Uwanja wa Taifa wana kazi moja tu ya kutafuta pointi tatu muhimu.

Simba itamenyana na Namungo ya Lindi Uwanja wa Taifa, mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kukutana kwa timu hizi mbili ndani ya ardhi ya Bongo.

Mkude amesema: "Tunatambua kwamba ligi sio kitu chepesi na kila timu ni bora kikubwa ambacho tunafikiria ni kuona namna gani tunapata pointi tatu ambazo zitatupa mwanga wa kule ambako tunakwenda," amesema.

Kwenye mechi mbili za mwisho wakati Simba ikikusanya pointi sita za kanda ya ziwa, Uwanja wa CCM Kirumba, Mkude alifunga jumla ya mabao mawili na alitoa pasi moja ya bao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic