MWAKA 2019 umeshameguka na sasa tupo mwaka 2020, leo ni Januari,29. Haya hapa ni matukio ya StarTimes 2019:-
Tangu kuingia katika soko la Afrika Mwaka 2018, StarTimes inajitahidi kufikia Malengo yake, ili kuhakikisha kwamba kila Familia ya Kiafrika inapata,nafasi na uwezo wa kuangalia/Kutazama Televisheni ya Kidigitali.
Na hivi sasa StarTimes inatoa huduma kwa watu takribani Milioni 30 katika nchi 37. Ukuaji huu mkubwa umeifanya StarTimes kuwa muendeshaji mkubwa wa runinga Barani Afrika na pia katika kuhakikisha inaleta maudhui mazuri kwa wateja wake.
StarTimes imetoa kipaumbele kwa jamii katika kuhakikisha inarudisha kile inachopata hasa katika kuunga mkono Taasisi zisizo za kiserikali, Sekta ya Filamu Afrika.
Mwaka 2019 StarTimes ilitoa mchango wake kwa Jamii katika haya:-
UCHANGIAJI
Polisi
Kampuni ya StarTimes Ilichangia Polisi vifaa vya Michezo ikiwemo Tshirt. Hii ilikua katika kuchangia jamii na kusaidia mahitaji mbalimbali.
Tokomeza Ziro
Vile vile StarTimes ilichangia Elimu katika kampeni ya TOKOMEZA ZERO, Kisarawe kiasi cha Shilingi Milioni 10 katika kusaidia Serikali kwenye jitihada za kuhakikisha inatokomeza Zero.
Afya
Pia iliweza kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 4 kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute at Muhimbili National Hospital. Pesa hizo zilitolewa kusaidia Matibabu pamoja na huduma nyingine kwa watoto wenye matatizo ya Moyo.
HUDUMA KWA JAMII
StarTimes iliweza kutembelea kituo cha watoto yatima kitwacho (CHAWAMA ) kilichopo Sinza ,na kuwapatia msaada kiasi cha Shilingi Milioni 3.
Kwa Upande wa Tamthilia mwaka 2019 StarTimes iliweza kuleta Tamthilia ya Waaris yenye maudhui yaliyopendwa na watazamaji wengi na imejichukulia umaarufu sana ikifuatiwa na Wild Flower, Blood Sister na The queen of Flow.
UDHAMINI
Mwaka 2019,StarTimes waliweza kudhamini tamasha la wasafi lililofanyika katika mikoa mitano na kumalizikia jijini Dar es Salaam, ilifanikiwa kudhamini mashindano ya kusaka vipaji ya Bongo Star Search ambayo yalikwenda vizuri na kuhitimishwa vizuri.
MATUKIO
StarTimes iliweza kufanya matamasha ya kuleta wasanii wa tamthilia ya Ode to Joy iliyofayika katika Hotel ya Hyatty iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
ni wasanii maarufu sana nchini China,Tamthilia hii iliweza kufanyiwa tafsiri kwa lugha ya Kiswahili.
TUZO
StarTimes imekabidhiwa TUZO kutoka Shirika la TACAIDS Tanzania kwa kutambua mchango wao StarTimes nao wakatoa mchango wa shilingi Million 5 ilikusaidia Serikali katika mapambano dhidi ya kutokomeza virusi vya Ukimwi.
0 COMMENTS:
Post a Comment