January 30, 2020


Uongozi wa Yanga umesema hawakubaliani na adhabu walizopewa na Bodi ya Ligi kwa wachezaji wao pamoja na klabu hiyo kwa ujumla tayari wameandika barua kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), CAF, FIFA, Takukuru na mamlaka nyingine kulalamika juu ya suala hilo.

Kamati ya Saa 72, Shirikisho la Soka Tanzania hivi karibuni ilitoa adhabu mbalimbali pamoja na
faini kwa klabu ya Yanga pamoja na wachezaji kutokana na makosa mbalimbali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), Steven Mguto alitangaza kuwafungia mechi tatu na faini ya
Sh 500,000 kwa wachezaji wa Yanga, Ramadhani Kabwili, Mrisho Ngassa, Cleofas Sospeter baada
ya kugoma kutoka uwanjani katika pambano la ligi dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa
Sokoine Mbeya.

Yanga pia ilipigwa faini nyingine ya Sh 500,000 baada ya kushindwa kuwakilisha kikosi chake
katika mechi ya ligi dhidi ya Tanzania Prison, lakini katika mchezo dhidi ya Simba Yanga
walipigwa faini nyingine ya Sh 200,000 kwa wachezaji na benchi la ufundi kushindwa kutumia
vyumba rasmi vya kubadilishia nguo na faini nyingine ilikuwa ya Sh 500,000 baada ya mashabiki
wake kuwarushia chupa waamuzi.

Akizungumza na makao makuu ya Yanga, Afisa habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema
Kamati ya saa 72 imeamua kuwafungia wachezaji wao pamoja na kuipiga faini timu kwa makosa
waliotaja mbalimbali.

"Yanga hatukubaliani na adhabu hizo kwani kuna mambo mengi ya kisheria hayakufuatwa mpaka
kuamua kutoa hukumu hiyo.

“Tulipeleka malalamiko yetu mengi kwa wasimamizi wa ligi ili hatukupewa majibu, kwa maana
hiyo tumeandika barua kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), CAF, FIFA, Takukuru na mamlaka
nyingine husika kulalamika juu ya hilo," alisema Bumbuli.

6 COMMENTS:

  1. Huyu Hasani Bumbuli ni Bumbula kweli. Yanga wanapoteza muelekeo na utashangaa kama Yanga kweli inaongozwa na Dokta Mshindo?kwani nani asiejua kuwa TFF,CAF,FIFA wanaongea Lugha moja. YANGA Kukimbilia FIFA ni kujivuruga,Wakae tu chini na TFF wayamalize kwa amani la sivyo watapata azabu kali zaidi na kama hawaamini wacha tu wakomalie FIFA.Unajua kuanzia suala la Zahera kuidharau TFF Yanga wakashangiria kwa vifijo na kumvimbisha kichwa Zahera. Lakini baada ya Zahera kuona ni m'babe kuliko TFF akaugeuzia ubabe wake na kiburi chake zidi Yanga yenyewe, na kilichotokea wao wenyewe Yanga wanajua.YANGA ni timu isio na nidhamu yaani hawapo professional kabisa kiasi cha kumfanya hata kocha wao mpya kuwashangaa.Leo Yanga wanatetea vitendo vya kijinga kwa wachezaji wao.Wapo tayari kwemda hata FIFA kutetea upumbavu. Hawa wachezaji wanaotetewa leo ndio watakao kuja kuitesa YANGA kesho kwa utonvu wa nidhamu. Hawa wachezaji ili kudumisha nidhamu ndani na nje ya klabu,Yanga ilipaswa kuwapiga faini kutoka kwenye mishahara yao ili iwe fundisho kwa wengine
    Ila kwenda FIFA kushitaki kuwa wachezaji wenu wameadhibiwa kwa ukosefu wa nidhamu ni sawa na kumshtakia Mungu kuwa umeibiwa pombe yako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah kweli we mkia wa level ya Phd, so wafurahie upuuz wa soka la tz vile linaendeshwa? Now ni tym ya kutafuta haki, waache waende, wakibamizwa na huko si wao, kwani we utaumia?

      Delete
  2. Unthinking respect for authority is the greatest enemy of truth,mjomba acha kufuata hisia zinazoonekana ni majority,in mediation you have to try to be different in views,that i mean mission and vission,yanga itaangamia kwasababu yakutokufuata taratibu za kisheria,hii ni kwasababu katika michezo ambayo ipo chini ya uratibu maalumu mfano ligi kuu ya vodacom mtu yeyote anapofanya kosa atahukumiwa kwakufuata sheria ndogo za bodi ya ligi ambazo zimewekwa na uongozi wa juu yani CAF,ambapo na CAF nao wamepewa muongozo na FIFA,na hii ndiomana ndugu hapo juu amesema TFF,CAF na FIFA wanatumia lugha moja,kwamaana utaongea na makaratasi yatakayokuonyesha taratibu zote.yanga kuweni makini sana katika hili,kama kawaida povu ruksaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  3. FIFA kubadili uamuzi wa kinanuni wa TFF ni ndoto za mwendawazimu.

    ReplyDelete
  4. Kweli ushabiki ni umbulula, mtoa hoja wa kwanza hapo juu hujitambui na hata hukumbuki unachokiandika msingi wake nini! Hivi si ndio nyie "simba" mliandika barua FIFA kulilia point 3 baada ya kuchapwa na Kagera wakati lilikuwa goli halali? Mlipata adhabu FIFA? Kwa nini kuzuia wengine wasitafute haki, au vile ulivyobugi unachukulia wote kuwa hivyo? Lahasha! Ligi sasa hivi inaendeshwa kwa misingi ya wanachama wa Simba, full kubebana mpaka inatia aibu!

    ReplyDelete
  5. Ndioo mpo sahiihi wote kila kitu c cha simbaa mfanoo jana duu simba hongereni wote ata saleh jembe pia nilikua napenda habari zako lkn ww pia mnafiki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic