January 30, 2020


BALAA walilokutana nalo Yanga ni kupigwa faini ya shilingi milioni 2.7 kutoka kwa Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya saa 72) iliyokaa Januari 20, mwaka huu kutokana na makosa mbalimbali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto aliweka wazi kwamba kikosi hicho kimepigwa faini ya shilingi laki tano baada ya kutowasilisha listi ya wachezaji wake walipocheza na Tanzania Prisons katika Uwanja wa Samora, Iringa Desemba 29, mwaka jana.

Prisons nao wamekumbana na faini hiyo kwa kuzingatia kanuni ya 14:3 juu ya taratibu za mchezo.

“Faini nyingine ya Yanga ni kutokana na mashabiki wao kurusha chupa uwanjani na kuwarushia waamuzi kwenye mechi yao dhidi ya Simba, Januari 4, adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni 43:1 kuhusu udhibiti wa klabu.

“Pia Yanga wamepigwa faini ya shilingi laki mbili kwa kutotumia chumba rasmi cha kubadilishia nguo, licha ya kulinda vyumba hivyo kwa siku tatu nzima. Kwenye mechi hii kuna matukio ambayo yalitokea na hayakuripotiwa, tutayapeleka kwenye kamati maalum, ambapo kwa faini hizo mbili wamepigwa rungu la shilingi milioni 1.2.

“Wachezaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, Ramadhan Kabwili na Cleophace Sospeter wamepigwa faini ya shilingi laki tano na kufungiwa mechi tatu baada ya kugoma kuingia vyumbani kwenye mechi yao na Mbeya City. Wachezaji wa Mbeya City Shaban Majaliwa na Kevin John nao wamekumbana na adhabu kwa kuzingatia kanuni ya 38:9 ya udhibiti wa wachezaji,” alisema Mguto.

Kwa adhabu hizo za Yanga wamepigwa faini ya shilingi milioni 2.7.

“Kocha wa Yanga, Luc Eymael amepewa onyo kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa juu ya masuala ya ubaguzi kwenye mechi yao na Azam FC, lakini pia tunawaagiza Yanga nao watoe tamko juu ya kocha wao huyo kutokana na suala hilo.

“Katika Ligi Daraja la Kwanza, Friends Rangers wamepewa pointi tatu na mabao matatu baada ya wapinzani wao Njombe Mji kuwa na wachezaji pungufu uwanjani.

“Njombe walikuja uwanjani wakiwa na wachezaji ambao hawakuwa wanafuzu kucheza katika mechi hiyo kwa sababu walisajiliwa dirisha dogo. Wakabaki wachezaji saba na bahati mbaya kipa wao akaumia akapelekwa hospitali wakawa sita wakashindwa kuendelea.

“Ligi Daraja la Pili, Mkamba Rangers wamepoteza mechi yao dhidi ya Villa Squad, baada ya kufanya udanganyifu wa leseni kwa kubandika sura za wachezaji wengine katika leseni za wachezaji wengine. Villa wamepewa pointi tatu na mabao matatu,” alisema.

8 COMMENTS:

  1. hizi adhabu hutolewa kwa Yanga tu au vile TFF wote ni Simba dam ???
    povu rukhsa

    ReplyDelete
  2. Timu ya wananchi,acheni kujiaminisha kwamba nyinyi ni zaidi ya serikali ya mpira(TFF CAF na FIFA),mtaangamia katika soka mnaweza mjikute kwenye adhabu ambazo zitagharimu maisha ya watu wengi sana,jaribu kua wastaarabu kwani kila sehemu kuna taratibu zake na endapo utaenda kinyume nazo basi itakua umejiweka mwenyewe kwwnye mazingira hayo mabaya,ni asubuhi tu tulikua hapa na mdahalo juu ya kitakachoipata yanga kama hawatafuata taratibu katika hizi changamoto wanazokumbana nazo,saa hii yanatimia.

    ReplyDelete
  3. Na hata huko mbele wanakoelekea yanga watapata pigo ambalo watakaa chini wajute sana,kwani suala lakwenda FIFA linaweza likafufua mengi sana yaliyojificha ndani ya yanga na hapo ndipo itakapo igharimu timu kwa namna fulani,chamsingi wapate picha halisi na waifanyie kazi,kwasababu kama TFF ameweza kukuhukumu kwakutumia vipengele vya sheria na kanuni za mpira ambapo muaandaaji ni CAF akipokea maagizo kutoka FIFA,sasa je ninyi mtatumia vigezo gani kwenda kuishinda TFF huko CAF na FIFA,na ikiwezekana basi ujue mtaishinda mpaka FIFA katika hili,tuiombee yanga maana hakuna simba imara bila yanga bora.

    ReplyDelete
  4. Mtani kwa hili ameteleza!!!

    ReplyDelete
  5. Tff unaangalia fani tu bila mshitakiwa kutoa maelezo.Kama kweli wanasimamia haki maamuzi ya Wawa wapo kimya? Sakata la arufu mbaya kwenye vyumba vya wapinzani wa simba lichukuliwi hatua? Mwamuzi Kati ya yanga na Mbeya cite tuliambiwa amepelekwa kwenye uchunguzi lakini Jana yuleyule kachezesha mechi ya Simba na Namungo na kaaribu tena.Hii Sasa hali mbaya kwenye mpira wetu

    ReplyDelete
  6. We cannot solve our problems with the same thinking we used to create them,waasisi wa haya matatizo ni sisi wenyewe hivyo kamwe hatuwezi kuyatatua kwa upeo wetu,mwanafunzi anafundishwa na mwalimu kwa dhamira yakufaulu mtihani lakin pale inapotokea mwanafunzi huyo amefeli hata kama ni kwa bahat mbaya(coincdnc) anaelaumiwa ni mwanafunzi,hii ni kwasababu mbona wengine wamefaulu?kumbe source of the problems is ourselves,kwanin nasema hivi??kwasababu kama umegundua shamban kwako kuna magugu ninachokijua mimi lazima utayaondoa tu ili ubaki na ngano kwa ajili ya palizi nakupata mavuno Yaliyobora.Yanga ingeondoa magugu Kwenye uongozi wake Ni ushauri tu.povu ruksaaaaa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic