February 26, 2020


IMERIPOTIWA kuwa uongozi wa Arsenal umeanza kufanya mazungumzo na nahodha wa kikosi hicho, Pierre- Emerick Aubameyang ili kuongeza mkataba ndani ya kikosi hicho.
Aubameyang awali alikuwa anataka kusepa ndani ya kikosi hicho kilipokuwa chini ya Kocha Mkuu Unai Emery ambaye alikuwa anahitaji huduma yake ndani ya kikosi hicho na kwa sasa timu ipo chini ya Mikel Arteta.
Raia huyo wa Gabon amekuwa imara ndani ya Arsenl tangu ajiunge mwaka 2018 ametupia jumla ya mabao 60 na kwenye Ligi Kuu England msimu huu akaunti yake inasoma mabao 17 na pasi moja ya bao.
Mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kuona namna gani watamshawishi nyota huyo mwenye miaka 30 ili abaki ndani ya kikosi na inatajwa silaha kubwa ipo kwenye kumuongezea dau kwani wakishindwa kupata saini yake huenda akasepa bure kwa kuwa mkataba wake unakaribia kumeguka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic