February 26, 2020


BAADA ya kikosi cha Simba kurejea leo Dar es Salaam kesho kinaanza maandalizi yao kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Jumapili.

Simba ilikuwa Shinyanga ambapo jana Februari 25 ilimenyana na Stand United kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora wa Kombe la Shirikisho na kupenya kwa mikwaju ya penalti 3-2.

Ndani ya dakika 90 Simba ilitoshana nguvu na Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwani bao lililofungwa na Hassan Dilunga wa Simba kwa penalti dakika ya 51 liliwekwa sawa na Miraj Saleh wa Stand United dakika ya 67.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa macho yao yote ni mbele ya KMC, mchezo wao wa ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic