February 2, 2020


JAFFARY Maganga,Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa leo watapambana mbele ya Mbeya City kuzisaka pointi tatu muhimu.

Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 leo itamenyana na Mbeya City Uwanja wa Samora, Iringa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Maganga alisema kuwa kila kitu kipo sawa na baada ya kulazimisha sare mbele ya Mtibwa Sugar watapambana kupata pointi tatu mbele ya Mbeya City.

"Mchezo wetu uliopita mbele ya Mtibwa Sugar tulibanwa na tulilazimisha sare ya kufungana bao 1-1, kwa sasa tunautazama mchezo wetu dhidi ya Mbeya City kiupekee na tutapambana kupata pointi tatu mashabiki watupe sapoti," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic