February 2, 2020

KOCHA wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa kila anapokuwa na mechi karibu huwa halali akikesha kutafuta mbinu za kuwamaliza wapinzani wake jambo ambalo linamsaidia kupata matokeo chanya.
Leo, Uwanja wa Taifa, Yanga itakuwa kibaruani kusaka pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar jambo ambalo limemkosesha usingizi Eymael ambaye anatafuta ushindi wake wa pili kwenye mechi za ligi alishinda mbele ya Singida United mabao 3-1 na alipoteza mbele ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 3-0 na mbele ya Azam FC kwa kufungwa bao 1-0.
Eymael amesema kuwa anatumia muda mwingi kuwasoma wapinzani wake ili kujua namna itakayomsaidia kupata ushindi jambo linalomfanya ashindwe kulala.
“Silali, kwa ajili ya Mtibwa, nakesha kufikiria namna gani tutaweza kupata ushindi kwenye mechi zetu zote bila kujali tunacheza na nani, kikubwa ninachokifanya ni kutafuta mbinu na sehemu ya kutokea kwani nina amini kazi itakuwa kubwa.
“Tulipotezwa nao tulipokutana nao kwenye Mapinduzi niliona ina wachezaji wazuri na wana vitu vya kipekee ila kwa sasa timu imeanza kupata matokeo maana yake tumeanza kuimarika,” alisema Eymael.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic