TIMU ya Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael ina vigongo vitatu vikali ambavyo ni sawa na dakika 270 kabla ya kukutana na watani zao wa jadi Simba, Uwanja wa Taifa, Machi 8.
Kwenye mchezo huo Yanga atakuwa mwenyeji akiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2, Januari 4 na Simba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Kazi ya kwanza itakuwa kwa Yanga kumenyana na Gwambina mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora itakuwa Februari, 26 ni baada ya jana kumalizana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani na kuambulia sare ya bila kufungana.
Kituo kitakachofuata kwa Yanga ni dhidi ya Alliance, mchezo wa Ligi Kuu Bara itakuwa Februari 29 Uwanja wa Taifa.
Itamalizana na Mbao kwanza Machi, 03 kwenye mchezo wa ligi kukamilisha dakika 270 kabla ya kukutana na Simba, Machi 8 Uwanja wa Taifa.








Gwambina anashinda tena goli tatu,atashinda mbele ya alliance then atasuluhu na mbao alafu akija kwa mnyama anachezea tatu au nne kocha atafukuzwa.WEWE MHARIRI HIFADHI MANENO YANGU NA SIKU YAKITIMIA UYALETE HAPA.
ReplyDelete#NAKUBALI
DeleteYanga hawawez kumfukuza kocha kwa sababu ameletwa na Gsm na hao GSM ndio wana sauti kwa sasa ndani ya yanga ni viongoz watajiuzulu wakiikimbia timu kwa sababu ya presha za mashabiki
ReplyDelete