February 24, 2020


DAVID Molinga kinara wa utupiaji ndani ya Yanga bichwa lake limekwama Uwanja wa Uhuru dakika 270 bila kucheka na nyavu.
Molinga ametupia jumla ya mabao saba ndani ya Yanga kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20.
Mara ya mwisho Molinga kufunga ilikuwa ni mbele ya Ruvu Shooting, Februari 8, Uwanja wa Uhuru ambapo Yanga ilishinda bao 1-0 lilifungwa na Molinga kwa kichwa akimalizia pasi ya Ditram Nchimbi.
Mechi tatu zilizofuata Molinga hakufurukuta ilikuwa mbele ya Mbeya City, Februari 11, kwenye sare ya kufungana bao 1-1, Februari 15,Yanga 0-0 Tanzania Prisons na Februari 18, Polisi Tanzania 1-1 hajacheka na nyavu.
Jana Yanga ilikuwa Uwanja wa Mkwakwani ikimenyana na Coastal Union, mchezo wa ligi Molinga hakuwa sehemu ya kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic