KELVIN Sabato mshambuliaji wa Kagera Sugar amekuwa mshambuliaji wa kwanza ndani ya mwaka 2020 kusepa na mpira wake kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na kufikisha jumla ya washambuliaji wanne waliosepa na mipira msimu wa 20219/20.
Sabato ambaye alisajiliwa na Kagera Sugar akitokea timu ya Gwambina inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ambayo ilimsajili kutoka Mtibwa Sugar, alifunga hat trick yake ya kwanza mbele ya Singida United kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba na ilishinda mabao 3-0.
Ditram Nchimbi alianza kufunga mbele ya Yanga wakati huo akiwa Polisi Tanzania na mechi hiyo iliisha kwa sare ya kufungana mabao 3-3, Obrey Chirwa alifuata mbele ya Alliance wakati Azam FC ikishinda mabao 5-0, Daruesh Saliboko wa Lipuli alifunga mbele ya Singida United na juzi Sabato alifunga hat trick ya kwanza kwa mwaka 2020 mbele ya Singida United wakati wakishinda mabao 3-0 Uwanja wa Kaitaba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Sabato amesema kuwa hakuna siri ya mafankio zaidi ya juhudi ndani ya Uwanja.
“Kikubwa ni kupambana na kujituma kwa ajili ya timu, kufuata maelekezo na kushirikiana ni nguzo ya ushindi ya ushindi kuhusu siri sina,” amesema Sabato.
0 COMMENTS:
Post a Comment