February 2, 2020


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union amesema kuwa kilichomponza kupoteza mchezo wake mbele ya Simba ni kukosa umakini kwa wachezaji wake na kuruhusu makosa.

Jana Februari, Mosi, Uwanja wa Taifa, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union na mabao yote yalifungwa na Mbrazili, Gerson Fraga.

Mgunda amesema:"Mpira ni mchezo wa makosa, vijana wamepambana kwa kadri ya uwezo wao mwisho wa siku wamefanya makosa na wapinzani wao wameyatumia.

"Kikubwa ambacho ninakwenda kukifanya ni kuyafanyia kazi makosa ambayo yamefanyika ili yasijirudie tena," amesema.

Ushindi huo unaifanya Simba izidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 47 huku Coastal Union ikiwa nafasi ya tano na pointi zake 30 na zote zimecheza mechi 18.

4 COMMENTS:

  1. Simba wapo kwenye mwenendo mzuri chini ya Matola na Sven tena sana ila kuna wapumbavu fulani wanataka kuitoa timu kwenye mstari. Namba hazidanganyi kwani takwimu zinaonesha kuwa Simba ya kocha mpya imekuwa ikibadilika kulingana na hali ya mchezo. Ukianagalia utaona kabisa kocha anapambana kutafuta na kuunda kikosi cha ushindani.Jambo Moja nimekuja kujifunza kutoka kwa kocha mpya wa Simba ni kwamba hampangi mchezaji kwa ukubwa wa jina lake na ndio maana kuna baadhi ya Mashabiki wa Simba wanapata taabu hadi kutaka kuandamana kwa ajili ya kocha ila kwa mtu mwenye akili timamu unakaa chini na kujiuliza hao mashabiki wa Simba wanaotaka kuandamana kwa ajili ya kocha wao wanachokitaka ni kitu gani? Au wanaajenda zao nyengine binafsi? Au kuna nguvu fulani kubwa ipo nyuma tao yakutaka kuihujumu timu katika wakati ambao Simba wanahitaji umoja zaidi kwanza kocha wao ni mgeni na mpya kabisa kimazingira ila unamuona kabisa jamaa ni mchapa kazi na nnaimani kabisa kama Simba watampa ushirikiano wa kutosha basi atawajengea timu yenye heshima kabisa. Hakuna binaadamu mkamilifu kila mtu ana mapungufu yake . Kila mtu anautamaduni wake wa kufanya kazi jamaa anaonekana ni mzungu mzungu kitabia na baadhi ya watu au wachezaji wanaweza kumuona mjeuri hasa kwa wale waliozoea kubembelezwa. ni kuwekana sawa na kuunda kitu kilicho bora kwa ajili ya taasisi la sivyo Simba itaendelea kufukuza makocha kila kukicha kwa kusikiliza mihemko ya baadhi ya mashabiki wake na wanachama wake. Timu imara haiundwi kwa mechi sita za ligi. La kushangaza kwanini viongozi wa Simba hawakemei baadhi ya Mashabiki wao wanaoendesha kamapeni inayombeza kocha wao wakati timu ikifanya vizuri tu. Kuna mashabiki wa Simba wanaamini timu yao inahaki ya kuifunga kila timu kwenye ligi kuu tena kwa magoli mengi? Ni ujinga kabisa kwani ukiangalia kwa makini timu nyingi za ligi kuu bara zipo vizuri na zina wachezaji wenye njaa ya maendeleo wakati wachezaji wa Simba wakijiona mabosi. Ushindani kwenye ligi kuu na ndio maana hata Azam wanateseka,Yanaga wanachemka.Kuna mashabiki wa Simba walisikika wakimlazimisha kocha kumpanga mchezaji fulani kwa kumtaja kwa jina kwa nini hampangi John Boko? Na kama vile kocha kakisikia wanachokililia kwani kwenye mechi coastal Union kocha akampanga Boko ila kazi ya Boko ikaenda kufanywa na mbarzli. Boko bado hajatengaa vizuri kutokana na majeraha.
    Hakuna timu ligi kuu inatengeneza nafasi za kufunga kama Simba tatizo lipo kwenye umaliziaji makini wa nafasi hizo na hii inaoanesha kocha na benchi lake la ufundi wapo vizuri katika majukumu yao.Ila kuna kitu Simba wanatakiwa kufanya hasa kwa upande wa Selemani Matola kwakuwa nnaimani anauzoefu zaidi mienendo wa soka letu.Amuangalie zaidi huyu Mbrazili Viera kisha azungumze na kocha wake mkuu kwani ukimwangalia Fraga utagundua kuwa anapokuwepo kwenye eneo la kumi na nane ni mtulivu wa ajabu na mara nyingi akichukua maamuzi ya jaribio la kufunga mara nyingi hufanya kwa kwa usahihi habahatishi kwa maana nyengine huyu ni fowadi ni mtambo wa Magoli uliopo chini ya watu wasiojua jinsi unavyofanya kazi. Kama huamini nenda kayaangalie magoli yote aliefunga Fraga viera tangu afike Simba basi utagundua yakwamba kama fowadi ya Simba inakuwa tulivu kama huyu jamaa basi Simba wasingehitaji fowadi mwengine kwa sasa na ni ushauri tu pengine utafika kwa wahusika na kuufanyia kazi. Mfano shomari kapombe ni kiungo mkabaji mahiri kabisa kila mtu anajua hilo. Hata shamte, Patric phiri alimtumia kama kiungo mkabaji na alikuwa akifanya vizuri tu. Kwa kifupi ubora wa kocha ni jinsi ya kumtafiti mchezaji wake na kumtumia kwenye namba sahihi kulingana na uwezo wake badala ya kukariri na namba za wachezaji.

    ReplyDelete
  2. Kabisa,vipi mbele akisimama kagere na Fraga kama fowadi pacha za kati,Kahata na Dilunga wakasimama wingi,chama na shibob ama Mkude wakasimama kati.utamalizia kwenye beki. Toa maoni yako...

    ReplyDelete
  3. Fraga hawezi kucheza kama mshambuliaji, inafaa abaki nafasi yake, kwanza ni mkabaji mzuri sana, mutu hapiti.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic