IMEELEZWA kuwa uongozi wa Mtibwa Sugar umewapa Sh milioni 70 wachezaji wake ili kuhakikisha wanashinda mechi zake za ligi ukiwemo wa leo dhidi ya Yanga.
Habari zinaeleza kuwa Sh milioni 50 zilitolewa na uongozi zilitokana na zawadi ya kutwaa Kombe la Mapinduzi na Sh milioni 20 zilitoka kwa uongozi wa juu na zote walikabidhiwa wachezaji wagawane.
“Wachezaji kwa sasa wamevimba mifuko wapo vizuri, fungu walilopewa sio la kitoto milioni 70 zisikie tu ila zote wamepewa wagawane lengo ni kuwaongezea morali kwenye mechi zetu zote ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Yanga,” kilieleza chanzo hicho.
Alipotafutwa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kwa kifupi: “Wachezaji wapo vizuri kwani walipewa fedha za kutosha baada ya kushinda Kombe la Mapinduzi ila suala la kiasi hilo tuliache, tunajua tutacheza na Yanga, hawa ndio hesabu yetu kubwa, wachezaji wametuahidi kutafuta matokeo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment