February 2, 2020


LEO Uwanja wa Taifa kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga iliyo chini ya Luc Eymael raia wa Ubelgiji na Mtibwa Sugar iliyo chini ya Zuber Katwila.

Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kutokana na matokeo ya timu hizi kwenye mechi zao zilizopita.

Msimu uliopita timu hizi zilipokutana kwa mara ya kwanza Uwanja wa Taifa Yanga ilishinda mabao 2-1 na zilipokutana mzunguko wa pili, Uwanja wa Jamhuri, Yanga ilifungwa bao 1-0.

Hawa hapa wataukosa mchezo wa leo kwa upande wa Yanga kwa mujibu wa Meneja wa timu Abeid Mziba, Mrisho Ngassa, ana adhabu ya kukosa mechi tatu, sawa na Ramadhan Kabwili pamoja na Anderw Vincent mwenye kadi tatu za njano.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar, Dickson Job ataukosa mchezo wa leo kutokana na kadi nyekundu aliyoipata mbele ya Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic