Serikal ya Jamhuri wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufuatilia kwa karibu malalamiko yote yanayotolewa na wadau wa soka mara kwa mara katika Ligi Kuu na ligi nyingine.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo iliyotolewa leo, Jumatano, Dk Mwakyembe ameliagiza Baraza hilo kutoa mrejesho wa agizo hilo ndani ya siku tatu.
“Wizara inaendelea kupokea tuhuma mbalimbali/uonevu katika mashindano ya Ligi mbalimbali za mpira wa miguu yanayoendelea nchini, lakini wdau hawaoni hatua zikichukuliwa mara moja na kupatiwa mrejesho,” taarifa hiyo imemnukuu Waziri huyo.
Wakati huo huo, Rais wa TFF, Wallace Karia ameiagiza Bodi ya Ligi kukutana na Kamati ya Waamuzi kutathmini mwenendo wa uchezeshaji wa soka nchini. Lengo la mkutano huo ni kuhakikisha malalamiko dhidi ya uchezeshaji yanafanyiwa kazi.
Walalamika Akina fulani kwanini wametupwa mbali na mnyama na huku wanalipa mabilioni kununuwa wachezaji na makocha wenye mbwembwe nyingi na baadae inabidi kuwatimua na Kununuwa wengine na huku bado Hakuna matokeo wanayotaraji na pia kusingizia eti Mnyama anapendelewa na kuwa marefa wapo upande wao na hicho ndio kisa hapana kingine
ReplyDeleteSamahani wana simba haina haja yakuchukua nafasi kuanza kulalama kama wenzetu,nadhan kwa macho yetu tumejionea hivyo tunawaomba muonyeshe utofauti kwamba nyinyi ni watu mnaojielewa NYAMAZAENI KIMYAA TUONE WATATULETEA VAR YA GOLI LILIOKATALIWA?.
ReplyDeletesaleh jembe acha ujinga walisababisha malalamiko haya hadi wazir kusema ni simba unaitajaje yanga katika hili
ReplyDeleteTatizo wanaolalamika siyo Simba bali Yanga wanaoandika na kuposti clips mbalimbali juu ya Simba. Nafikiri tukae kimya na tujue mstakabali ni nini? Offiside trick ina mbinu nyingi na sisi wa nje tunaona upande mmoja tu.
ReplyDelete