February 26, 2020


HASSAN Dilunga amesema kuwa kikubwa anachokifanya ndani ya Simba ni kutimiza majukumu yake ya kazi anayoipenda muda wote.

Dilunga jana alifunga bao la kuongoza la Simba kwa penalti dakika ya 51 mbele ya Stand United na halikudumu baada ya Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kuweka mzani sawa dakika ya 67 kupitia kwa Miraj Saleh.

Kwenye hatua ya mikwaju ya penalti Simba ilishinda penalti 3-2 na kusonga mbele hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho huku Dilunga naye akifunga moja ya penalti kati ya hizo tatu zilizofungwa.

Wafungaji wengine walikuwa ni Chama na Deo Kanda.

Dilunga amesema:-"Furaha yetu ni kuona tunapata matokeo na kinachotubeba ni ushirikiano bado tuna kazi kubwa ya kufanya kikubwa sapoti kwa mashabiki,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic