HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa wachezaji wake wanapambana kiasi cha kutosha ndani ya Uwanja jambo linalomfurahisha.
Thiery jana timu yake imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wachezaji wake wanafanya kazi kubwa wanastahili pongezi.
"Wachezaji wanatimiza majukumu yao kwa kiasi kikubwa licha ya kwamba tunapitia kipindi kigumu hasa kwenye ratiba yetu, nina amini tutaendelea kupambana ili kuwa bora.
"Ligi ina mechi nyingi nasi tunajitahidi kwenye kila mechi kufanya vizuri," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment