February 7, 2020


Kocha wa Klabu ya Yanga, Luc Eymael, amesema kuwa kulikuwa na harufu kali na isiyoeleweka katika vyumba vyao vya kubadilishia nguo juzi Jumatano, Februari 6, 2020, katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi  ya Lipuli FC.

Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Lipuli, mabao ya Yanga yakifungwa na Mapinduzi Balama dakika ya 14 pamoja na Bernard Morrison dakika ya 31 huku bao la kufutia machozi la Lipuli likifungwa na David Mwassa dakika ya 58.

“Nimeona kipindi cha kwanza kizuri cha Yanga, tulipaswa kufunga magoli matatu au manne…..” alisema Luc.

Aidha, Kocha wa Lipuli Julio Ellieza alisema; “Wametunyima goli dhahiri shahiri, mpira kipa kadakia ndani…. mwamuzi kautoa kuwa kona.”

“Tumefanya makosa, tumeadhibiwa, tunakubali tumefungwa,” alisema Nahodha wa Lipuli FC, Paul Nonga na kuongeza kuwa mpango wao wa kipindi cha kwanza ulifeli ndiyo maana wakafungwa.

Yanga sasa imefikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 17 huku Lipuli ikisaliwa na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 19.

8 COMMENTS:

  1. Ama hii la harufuu kali ambayo anakiri kocha kuwepo ni tosha kuwa wanalogana Hawa wenyewe. Na kubwa linalowaumiza hawa jamaa ni ile Mnyama kuwa Ana mashabiki wengi zaidi Africa ukizitoa nchi chache mfano Misri na jinsi ilivopandishwa juu kimataifa na kumiliki viwanja vya hali ya juu. Hii no hasadi. kubwa Sana na itazidi kuwatesa

    ReplyDelete
  2. TFF nunueni LITMUS PAPER kuna timu inatumia kila mbinu, marefa,wachezaji hadi vyumba vya kubadilishia nguo. Mmh ilikuwa inashangaza watu wanapigwa hamsa away tena kwa huruma home wanashinda!!! Ilikuwa ni ngumu kuingia akilini. Hamna soka la namna hiyo. SOKA NI SCIENCE. Hii lazima tuikemee kwa nguvu zote!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Akili zako hazina tofauti na vyura wa pale jangwani kariakoo ambao kila siku wanashinda wanakoromaaa.Kama mna ushahidi kwanini msitoe hadharani...mnaogopa nini kutoa ushahidi kama mna vidhibitisho?Mie Nina wasiwasi na hawa wenyewe vyura ndio wanafanya haya Mambo.Alibi mnayo wenyewe.

      Delete
  3. unajua hapa Saleh Jembe kuweka habari kuwa kocha kasema kitu fulani haina kidhibitisho kuwa kweli kasema.hizi ni propaganda zile zile za Zahera aliaanzisha kwa AS Vita eti Simba inapuliza dawa.Kesi ilenda CAF...Wameona propaganda ya Simba ananunua marefa imekosa mshiko kwani marefa wanavuruga kati ya Azam na Prison, Mtibwa na Ruvu na sio mechi ya Simba pekee,Hata juzi wamezawadiwa ushindi kwa marefa kuwanyima Lipuli bao huku wakipewa kona.Imeishaonekana dhahiri bao la Yanga dhidi ya Prison ilikuwa offside na ile penalti haikuwa halali.Sasa ni nani anayenunua marefa.Au ni nani alishaingia kwenye historia hadi kufungiwa na CAF kwa kununua marefa.Si Yanga walirinda chumba chao siku 3 mfululizo kwenye mechi ya Simba..nini kinawazuia kufanya hivyo sasa kama wanajua vyumba vinapulizwa..Harufu ni sawa na macho ya muhusika anaweza ona cheini ni hiridhi..na harufu ya mayai yaliyooza mwengine atasema inanukia pafyumu..hamana namna ya kudhibitisha harufu mbaya ni mbaya kwa kila mtu..eti timu yao ilirudi imechoka..Ni Lipuli waliorudi wakijua wamepoteza na hawana cha kupoteza zaidi..hivyo walicheza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wenye historia ya kuhonga marefarii ni Yanga na sijui kama hawa mashabiki maandazi wanajua kuwa kuna records za Issa Makongoro na mwenzake walipigwa ban 5 yrs Kwa kutaka kuwahonga waamuzi waethiopia pale New Africa hotel na brief case yao.Tafuteni records TFF enzi hizo FAT

      Delete
    2. Naunga hoja yako.Hizi ni propaganda za kuichafua Simba brandy na kinachonisikitisha ni kuona viongozi(board of directors) wa Simba kutochukua hatua za kisheria Kwa kuwashtaki tena kwenye commercial court maana hawa wazushi wasio na ushahidi wana damage brandy ya Simba.Simba ina mwekazaji,wanahisa,wadhamini ambao wanatangaza bidhaa zao kupitia nembo ya Simba na hii ni biashara.Ombi langu kwa viongozi wa Simba chukueni hatua ya kudhibiti hizi propaganda.Wacheze Yanga na Lipuli eti Simba imepulizia madawa.Too much propaganda na Kwa kweli imeshakuwa kero Kwa wekundu wa msimbazi

      Delete
    3. Ukiona kimya ujue nafsi zinawasuta. Uzuri wa watu weupe ni BLACK OR WHITE tungewaiga tungekuwa mbali. Harufu haina kificho. Hizi ni mbinu chafu ambazo siyo Club ila watu wachache wanaonufaika na club wameamua kuichukua ili wapenzi wandanganyike watu wapige pesa. Hamuwezi kupigwa nyie bao tano za huruma arafu mje mshinde hapa. Ingekuwa hivo basi Taifa Stars ingeifunga Brazil uwanja wa Taifa. Wakalalamika tukaona waongo. What goes around comes around.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic