February 7, 2020


Baada ya kikiso cha Simba kuonesha kiwango kilicho butu katika mechi za hivi karivuni, inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wapo kwenye mchakato wa kusaka Kocha mwingine.

Timu hiyo inayonolewa na Sven Vandenbroeck ambaye ni raia wa Ubelgiji, imekuwa ikipata matokeo ya kusuasua tangu aanze kuinoa jambo ambalo limeanza kuleta wasiwasi katika mechi za ligi na mashindano ya kimataifa hapo baadaye.

Tetesi zilizopo hivi sasa ni kuwa mabosi Simba wanatajwa kutaka kumleta Kocha wa As Vita, Jean Florent Ibenge ili kuchukua majukumu ya Sven.

Taarifa za ndani zinasema uwezekano mkubwa wa Sven kufutwa kazi upo kutokana na uongozi wa juu, mashabiki na hata wanachama kutofurahishwa na namna mwenendo wa timu hiyo unavyoenda hivi sasa.

Sven alichukua nafasi ya kuinoa Simba baada ya kufutwa kazi kwa Patrick Aussema aliyekuwa akiinoa timu hiyo.

7 COMMENTS:

  1. Kama uushindi mnapata kiharali Sasa mnamfukuza kocha wa Nini?

    ReplyDelete
  2. Kocha Simba hana tatizo lolote na hata akiletwa kocha wowote kwa sasa pale Simba wasidhani mambo yatakuwa rahisi hivyo. Kwani inajulikana wazi kuwa kocha huyu anahujumiwa ili aonekane hafai. Kuna baadhi achezaji wakishirikiana na baadhi ya viongozi wanashirikiana kumuhujumu kocha ili aonekane hafai ila hizo ni zambi zitakuja kuwatesa Simba. Manchester United,Arsenal na Chelsea wanateseka hadi leo. Matatizo ya viongozi kushindwa kufanya usajili wa maana katika maeneo husika yanayowatesa Simba kwa muda mrefu,matekeo yake zigo anaangushiwa kocha. Kocha huyu huyu wa Simba anaeonekana m'bovu kama atakabidhiwa Namungo kwa vijana wale jinsi wanavyojituma na Simba waendelee na wachezaji wao hao waliolewa pesa na kujiona mabosi basi nakuhakikishia namungo watamalizia pazuri mwisho wa ligi kuliko Simba hii. Kwanza kabisa kuna uwezekano mkubwa kabisa Patrick Ausems na genge lake wana mkono wao kwa asilimia kubwa kuhahakisha kuwa kocha huyu anafeli. Ila Simba wahakikishe wanamlipa huyu kocha stahiki zake pindi wakiamua kuachana nae isiwe mambo ya kupelekana FIFA. Kocha anaambiwa mbaya wakati timu inaongoza ligi kwa point 12.

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeongea ukweli mtupu ndani ya Simba kuna shida ila tunaoumia ni sie hatuelezwi ukweli ila kiukweli wachezaji wanacheza chini ya kiwango ili tu aonekane kocha mbaya hatuezi endesha timu kwa kumuingilia kocha kazi yake ni shida kubwa hii ila ngoja tuone mwisho wake.

      Delete
  3. Kama simba watabadili tena ina maana viongozi wa simba wanafanya mambo ya kubahatisha. Kibinafsi kocha anajua anachofanya na unaona kabisa anajiamini akisuka kikosi imara ambacho hakuna mchezaji atakayejiona bora kuliko wengine. Na hii inahimarisha nidhamu ya timu.

    ReplyDelete
  4. Hao mashabiki wa Simba wanaoamadamana kuhusu kocha wao, wanatumika bila ya wao wenyewe kujijua na kuisaliti timu yao kwa faida ya watu fulani. Wao wenyewe hawashangai wanaandamana kuwasaidia wapenzi wa wanga kuizodoa timu yao lakini hakuna hata kiongozi mmoja anaekemea. Hata Manara kakaa kimya ujue kuwa kunazengwe hapo kocha kajengewa. Wachezaji wa Simba hawamtaki kocha kwa sababu ni wavivu wa mazoezi. Jamaa yupo serious. Yanga kinachowasaidia sio Mzungu ni Mkwasa kwani anajua soka la Bongo ni mazoezi ufundi wa kuchapia. Kocha huyu akiondoka hao wanaoandamana watakuja kujuta. Kocha akiondoka Simba hivi sasa hana cha kupoteza kwani muda mfupi tayari ameshajitengenezea C.V na watakaopoteza ni Simba sio yeye. Kinachotizamwa tangu aje Simba ameshinda mechi ngapi? Amepoteza ngapi?hayo sijui mambo ya offside ni mambo ya vijiweni lakini vitabuni jamaa yupo kwenye rikodi bora tangu atuwe Simba. Akiondoka ana uwezo wa kuomba kazi au pengine hivi sasa tayari kuna timu zinamuhitaji tayari. Kocha wa dizaini yake anahitaji muda ili kufaidi matunda yake. Kama ningekuwa viongozi wa simba ningemuacha kocha mpaka mwisho wa msimu na timu ikishindwa kuchukua ubingwa fukuza wachezaji karibu wote na kutafuta vijana wengine wapya makini kabisa wa kazi ambao kwa kiasi kikubwa liwe chaguo la kocha mwenyewe. Na ni vizuri hata kuwaataarifu wachezaji kwamba e bwana e kocha haondoki ila msimu ukishia vibaya tutaifumua timu nzima kuunda kikosi kipya. Kwa sababu hii tabia ya wachezaji kumuhujumu kocha ni tabia ya hatari sana kwa afya ya timu.Isitoshe kila kwenye mechi ya simba,Yanga wanamaliza kufuru zote kuhakikisha Simba inadondosha points,kuanzia kuipa sapoti ya siri na dhahiri timu pinzani inayocheza na Simba kihali na mali hadi kusaidia ushirikina, utaona hata police walipita mlango wa nyuma walipoingia kucheza na Simba. Ile sio akili ya kipolice kuamini ushirikina bali walishikwa sikio na mtani. Ila kila Yanga wanapojaribu kuzicheza mechi za Simba wanashangaa kwsni kimauzauza tu Simba anakuja kuibuka na ushindi kitu hicho Yanga kimewakera sana hadi kuonesha chuki za wazi kabisa ila mpira wa bongo hata waamuzi nao hupigwa kafara wakazibwa na macho wakapumbazika,wee acha tu. Uchawi huu wa kuizuia Simba tuuhamishie Taifa stars tufuzu world cup tatatataa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndg umendika vyema kisha mwisho ukharibu.
      simba akiacha kujiona mkuu atakuwa mshindani

      Delete
  5. Tabia ya kubadili makocha kama nguo itaiweka simba sehemu mbaya kuliko ilipo kwa sasa
    Mchezaji kupiga pasi hadi golini lakini hafungi gori hilo kosa la mchezaji sio kocha.

    Hakuna kocha bora bila wachezaji kutumia uwezo wao na maarifa ya kocha kupata ushindi uwanjani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic