February 15, 2020


Akijiandaa kuwavaa wapinzani wake Tanzania Prisons, Kocha Mkuu wa Yanga Mbelgiji Luc Eymael amesema mbinu alizozitumia katika michezo iliyopita waliyokutana hatazitumia tena na badala yake ataingia kivingine ili kuhakikisha anapata pointi tatu.

Kauli hiyo aliitoa kocha huyo ikiwa ni siku moja kabla ya kuvaana na Prisons, leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam saa 1 Usiku.

Katika mchezo huo, Yanga watakutana na ushindani mkubwa kutokana na kuwafunga Prisons mara zote mbili walizokutana kwenye ligi na Kombe la FA.

Luc alisema anatarajia kupata ushindani mkubwa katika mchezo huo kutokana na wapinzani wao kutokubali kupoteza kwa mara ya tatu mfululizo.

Luc alisema katika mchezo huo ataingia uwanjani na mbinu mbili tofauti za kuwavaa Prisons baada ya kuona moja waliyoingia nayo kushindwa kufanya kazi kutokana na wapinzani wao kuzisoma mbinu zao walipokutana.

Aliongeza kuwa hautakuwa mchezo mwepesi kwa kwao, lakini kutokana na maandalizi aliyoyafanya kwa kuboresha safu yake ya ulinzi na ushambuliaji anaamini atapata ushindi, kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani.

“Katika msimu huu tumekutana mara mbili na Prisons, hivyo tunaamini tayari wamezijua mbinu na mifumo tunayoitumia, hivyo basi kama kocha tutaingia kwa tahadhari kubwa katika pambano hili.

“Kikubwa tutaingia kwa mbinu mbili na tutazibadilisha baada ya kuona tulioingia nayo wapinzani kuijua, hivyo haraka tutabadilisha na kutumia nyingine mpya ambayo ninaamini itatupa ushindi.

“Mchezo huu siyo mwepesi kwetu, kwani wapinzani wetu hawatakubali kufungwa kwa mara ya tatu mfululizo ni lazima waje kivingine na kutuzuia kupata ushindi hapa nyumbani, hivyo tumejiandaa katika hilo,” alisema Luc.

2 COMMENTS:

  1. Prison ni kibonde wa Yanga kila mtu anajua. Na si kwa mpira bali prison hata iwe nzuri vipi ikicheza na Yanga hujilegeza sijui kuna siri gani ndani yake.labda kuna baadhi ya viongozi ndani ya timu yao ni mali ya Yanga.

    ReplyDelete
  2. Vipi ni kibonde wa Yanga au ameonyesha mpira?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic