Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck, ameweka wazi kwamba kwa sasa anachokifanya ni kuwachanganya wapinzani wao kwa kuhakikisha kila nyota wake kikosini hapo anafunga na siyo kumtegemea staa wao, Meddie Kagere pekee.
Mbelgiji huyo ameweka wazi hilo baada ya kumalizika kwa mechi yao na Coastal Union, Jumamosi iliyopita ambapo kwenye mechi hiyo Simba walishinda kwa mabao 2-0. Mabao yote yalifungwa na kiungo mkabaji Gerson Fraga.
Kagere ndiye kinara wa mabao ndani ya Simba ambapo hadi sasa amefunga 12 huku akiwa na asisti nne, huku akifuatiwa na Miraji Athuman ‘Sheva’ mwenye mabao sita.
Sven amesema kuwa kwa sasa anachokifanya ni kubadilisha wafungaji wake huku akimtaka kila mchezaji wake kuwa na uwezo wa kufunga na kutotegemea mabao ya Kagere tu.
“Hiki ni kitendo kizuri kuona kila mchezaji ana uwezo wa kufunga hapa na kutomtegemea mtu mmoja au wawili pekee kwenye suala hilo.
“Tazama kwenye mechi hii, mchezaji ambaye amefunga ni kiungo mkabaji, hiki ni kitu kizuri na tunatakiwa kukiendeleza kwa kila mmoja kufunga bila ya kujali ni beki, kiungo au mshambuliaji.
“Ninachokifanya ni kufundisha kila mmoja kuwa na uwezo wa kufunga na siyo kuwategemea watu wachache kwenye timu, ninataka kila anayepata nafasi awe na uwezo wa kufanya hivyo,” alisema Sven.
Huyu ndie kocha wa kweli asiye na majisifu, mbwembe na ahadi nyingi na kufanya kazi Bila ya kupiga makeleke
ReplyDeletehapo kocha nimemuelewa
ReplyDelete