February 2, 2020

MOHAMED Salah, raia wa Misri mshambuliaji anayekipiga ndani ya Klabu ya Liverpool ameendeleza urafiki wake na nyavu kwa kuwatungua Southampton mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Liverpool ikiwa Anfield, ilishinda mabao 4-0 na kuifanya izidi kujikita kileleni kwenye Ligi Kuu England.

Mfungulia balaa ndani ya Liverpool alikuwa ni Alex Oxlade -Chamberlain dakika ya 47 na Jordan Henderson dakika ya 60 huku Salah akikamilisha hesabu zake dakika ya 71 na 90.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kucheza jumla ya mechi 25 bila kufungwa, ikishinda 24 na sare moja ya kufungana bao 1-1 na Manchester United, imejikusanyia jumla ya pointi 73.

Bingwa mtetezi Manchester City yupo nafasi ya pili akiwa nyuma Kwa mchezo mmoja na ana pointi 51 kibindoni, tofauti ya pointi 22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic