February 16, 2020


Kipa namba moja wa Yanga, Farouk Shikalo amerudishwa kikosi cha kwanza jana Jumamosi dhidi
ya Prisons baada ya kukalishwa benchi kwenye michezo sita ya Ligi Kuu Bara.

Yanga jana ilimenyana na Prisons kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo
uliomalizika kwa sare ya 0-0.

Kwa mujibu wa kikosi kilichotolewa na benchi la ufundi la timu hiyo Shikalo alianza na Juma
Abdul, Adeyum Saleh, Lamine More, Ally Mtoni, Papy Tshishimbi, Mapinduzi Balama, Mohammed Issa, Yiype Gislain, Tariq Seif na Benard Morrison.

Shikalo mara ya mwisho kucheza kikosi cha kwanza ni mchezo wa ligi kati ya Yanga na Azam FC
ambapo mchezo ulimalizika kwa timu hiyo kukubali kipigo cha bao 1-0 bao lililofungwa na Ally
Mtoni.

Tangu hapo hajacheza michezo sita ambayo ni dhidi ya Singida United, Prisons, Mtibwa Sugar,
Lipuli FC, Ruvu Shooting, Mbeya City na jana ndio alipata nafasi ya kukaa golini mchezo dhidi ya
Prisons.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic