MTIBWA Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila haijafunga bao ndani ya mechi saba za mwezi Februari kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na imeambulia pointi moja.
Mara ya mwisho Mtibwa Sugar kufunga bao ilikuwa ni Januari 30, kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC Uwanja wa Uhuru, lilifungwa na Ismael Mhesa, baada ya hapo haijaambulia bao zaidi ya sare na kupoteza kwenye mechi zake saba ilizocheza sawa na dakika 630.
Februari 2 ilifungwa na Yanga bao 1-0, Februari 5 ilifungwa bao 1-0 na Ruvu Shoting Uwanja wa Mabatini, Februari 8 ilifungwa bao 1-0 na Lipuli, Uwanja wa Gairo, Februari 11 ilifungwa mabao 3-0 na Simba, Uwanja wa Jamhuri.
Februari 15 ilifungwa bao 1-0 na JKT Tanzania, Jamhuri, Dodoma, Februari 19 ililazimisha sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na ilifunga mwezi Februari kwa kufungwa bao 1-0 na Mbeya City Uwanja wa Sokoine.
0 COMMENTS:
Post a Comment