February 3, 2020




NA SALEH ALLY
NATAKA niende moja kwa moja kuwa nimekuwa nikikerwa na propaganda zinazoenezwa na baadhi ya watu ambao ninaamini wameshindwa mambo.


Mjadala huu unachombezwa na baadhi ya mashabiki ambao wanaonekana wameshindwa kujitambua, wameshindwa kuelewa kuwa wanatumika vibaya na baadhi ya viongozi ambao wameshindwa majukumu yao.


Kuna propaganda ambayo haina faida na afya ya mchezo wa soka nchini kuendelea kulazimisha ionekane waamuzi wanaipendelea sana Simba.


Katika hali ya kawaida, mimi kama mdau wa mpira siwezi kuungana mkono hata kidogo na waamuzi ambao ningeona wana nia hiyo.


Kama wangekuwa kweli wanaipendelea Simba, bila shaka tungepiga kelele na kukemea kwa kuwa kukua kwa mpira wa Tanzania, suala la haki linatakiwa kuchukua nafasi kubwa sana.


Binafsi ninapinga kama kweli kuna waamuzi wana mawazo au nia ya kutaka kuipendelea timu fulani ambalo si jambo sahihi na halina msaada hata kidogo kwa maisha ya ukuaji wa mpira wa Tanzania.


Pamoja na hivyo, nataka kuwaasa wale ambao wamekuwa bendera fuata upepo, wanalibeba suala hili bila ya kuliangalia kwa kina.


Simba ambayo sasa imefunga mabao 40 katika mechi 17, imependelewa mangapi ambayo wanaweza wakayaelezea na kuwaaminisha watu.


Tumeona waamuzi hawa wanakosea katika mechi hata zinazoihusisha Yanga na timu nyingine na si Simba tu, tumeona wanakosea hata katika mechi za Azam FC au za timu nyingine na wachezaji au viongozi wa timu za Ligi Kuu Bara wanalijua hili.


Simba imefunga mabao 40, ukiangalia  Yanga wamefunga 20, baada ya bao la jana dhidi ya Mtibwa Sugar, Lipuli wana mabao 23, Azam FC yenye 22. Tuambiwe kwa takwimu Simba kapendelewa mara ngapi badala ya hadithi tu.


Kwangu suala la Simba kapendelewa kama hakuna takwimu basi inakuwa ni kubabaisha tu mambo na kutaka kuhamisha hoja ya msingi ambayo tunapaswa kuizungumza.


Mimi nimesema waamuzi wanakosea katika mechi nyingi hata zile ambazo haziihusishi Simba na tunaona. 


Maana yake hapa, hoja ya msingi ni suala la waamuzi kuwa na kiwango duni katika utekelezaji wa kazi zao na hapa ndipo tunapaswa kupashikilia kwa ajili ya mpira wa Tanzania.


Tupunguze ushabiki katika mambo ya msingi, kila mara nimekuwa nikisema hakuna timu inayomiliki waamuzi na wanapokuwa wanavurunda, sote tunafahamu wapi pa kwenda na kuwakumbusha kuwa mambo yanaharibika.


Kuendelea kulia Simba inapendelewa wakati waamuzi wanakosea, ni kufunika makosa yao kupitia ushabiki, huenda kutengeneza hisia za wengine pia kupendelewa ili tuwe na ligi ya wanaopendelewa tu, jambo litatufanya tuwe na akili za hovyo kabisa.


Waamuzi wanavurunda na hili ndilo suala linatakiwa kufanyiwa kazi, wapate maonyo au kuchukuliwa hatua kali kwa wale wote wanaoboronga.


Unaona mechi ya watani Yanga na Simba, bila ya ubishi, ilionekana penalti waliyopewa Simba ina utata na kweli haikuwa penalti na hili ni kosa la ‘assistant line two’. Bao la pili la Yanga nalo lilikuwa na makosa sahihi kusema si bao kwa kuwa Mohamed Issa Banka alimsukuma kabisa Mohamed Hussein Zimbwe aliyejifunga lakini ‘assistant line two’ huyohuyo akajikausha ili kufunika kosa la kwanza kwa ‘kubalansi’.


Hii maana yake, hawa waamuzi wanajua matatizo yao na wanachokosea. Hivyo tusiwape nafasi kabisa ya kuendelea kurekebisha makosa yao kupitia makosa, wataziumiza timu.


Maana timu moja itaumizwa kwa makosa na udhaifu wa ubora wa mwamuzi halafu yeye atajirekebisha kwa kuiumiza nyingine tena, hii si sahihi.


Kwa sasa si nani anapendelewa kwa kuwa tukiangalia hivyo, hata wale wanaolalamika wanaweza kukuta timu yao imependelewa zaidi kwa udhaifu wa waamuzi au makusudi.


Hivyo vizuri kudhibiti pale yanapoanza kutokea maji kuliko kusubiri yatoke halafu tuanze kuchota kuyapunguza.


SOURCE: CHAMPIONI



13 COMMENTS:

  1. umejua kunifurahisha saleh jembe yaan umeongea ukwl kbs hlo ttz la waamuz

    ReplyDelete
  2. Mimi ni Yanga lakini nakubaliana na hoja ya Saleh Jembe tusihamishe magoli kwa kisingizio kwamba Simba inabebwa. Simba haibebwi.Mrefa wanafanya makosa kwenye mechi nyingi.

    ReplyDelete
  3. Lakini umeandika kana kwamba ni maoni ya wengi wakati ni maoni yako yanayowakilisha vile wewe binafsi unavyoona na wala sio Blogu nzima ya waandishi wa salehjembe

    ReplyDelete
    Replies
    1. si kweli!soma maoni ya wadau mtando huu..angalia maoni ya youtube..hata Mkwasa kwenye pre match alikiongelea hiki akidai Simba wanapewa penalti..sasa katika hayo 40 mangapi ni ya penalti..Kocha mkuu Yanga imekuwa kawaida yake kupost twiter. Tatizo inafanya waamuzi wanaanza kukataa penalti halali na magoli halali na Yanga ambao wanfunga moja au mbili kila mechi ndiyo wataathirika zaidi.ukianzisha mto ujue jinsi utauzima.swali ni katika hayo 40 ni mangapi ni ya penalti za kupewa na ni mangapi ni off side zilizoachiwa. Je tukifuta hayo aliyopendelewa Simba kuna uwezekano Yanga au Azam wakaizidi Simba mabao au points

      Delete
  4. Nani asiyekujua kama wewe Saleh Jembe ni Simba,maelezo yako yote ni kuitetea Simba,lakini nataka nikuambie kupendelewa Simba na marefa c kupewa maholi yasiyo ya haki tu,kuna mambo mengi uwanjani yanatendeka kuiuwa timu inayocheza na Simba,mpira unachezwa uwanjani na sikuhizi hata km hutoenda uwanjani basi kwenye runinga utaona,Wewe Simba endelea na usimba wako,lakini usitake kutuziba midomo kusema Simba inabebwa.

    ReplyDelete
  5. Saleh jembe kwanza Happy Birthday. Niliona nakala yako iliyoamabatinishwa na picha yako binafsi kuwajuza wasomaji wako juu ya uzaliwo wa Saleh jembe lakini cha kushangaza sikuona hata comment moja ya kukutakia kheri isipokuwa lawama tu, naamini licha ya mapungufu machache ya kibinadamu katika utendaji wa kazi zako lakini kiukweli kabisa unastahili pongezi sana kwa kuilea hii blog kusimama hadi leo naweza kusema Saleh jembe ni moja kati blog chache halisi ya michezo iliyosalia hewani nchini hongera sana.Wako wapi akina shafii Dauda na wengine wengi.Ukiangalia watanzania kula kukicha tumekuwa watu wa kukosa shukrani na ni jambo la hatari sana.Na tukitoka kidogo kwenye michezo wacha tupapase kidogo kwenye siasa na ni kuhusu mwanamichezo mwenzetu Ndugu Paul Makonda.Tumeona baadhi ya watu,Magazeti,waandishi wa habari na wanasiasa wa kitanzania wakifurahia habari za yeye kupigwa Marufuku kuingia Marekani? Kwanza Makonda hana shida ya kwenda Marekani ila lengo kuu hapa ni kuichafua Tanzania na serikali ya Magufuli ila haya Mambo yalishatabiriwa kutokea juu ya Magufuli na harakati zake za kuimilikisha Tanzania wataanzia wanyonge. Lakini huyu Makonda ndie aliejitoa Muhanga kupambana na Madawa ya kulevya,Makonda huyu ndie alielituliza jiji la Daresalam kutoka kwenye matukio ya kijambaazi ya kutisha ya mara kwa mara,Makonda huyu ndie aliewaunganisha watanzania wa madhehebu mbali mbali ya kidini na kuwa kitu kimoja,Makonda huyu ndie anaesimamia vipaji vya sanaa na michezo kwa vijana wa kitanzania moja kwa moja kutoka kwake yeye mwenyewe binafsi,Makonda huyu ndie anaepigana kuhakikisha hali za kinamama wanyonge zinapatikana,Makonda huyu ndie anaepigana kuhakikisha haki za watoto wazururaji mjini zinalindwa,Makonda huyu ndie kiranja mkuu anaesimamia kulipaisha jiji la Daresalam kuwa la kisasa zaidi Africa na mambo mengine mengi mazuri si rahisi kuyataja yote hapa anayofanya Makonda.Lakini inatokea nchi ya kigeni bila ya kufuata sheria za kimataifa kwa kutumia ubabe wake tu inatumia nguvu zake binafsi inajaribu kuiaminisha Dunia kuwa huyu ni mtu Mb'aya,hafai na sisi watanzania tunashangiria mikundu wazi juu kabisa hewani? Kwa kweli watanzania tujitafakari.Mabebebru hawa waliidanganya Dunia na kuwalaghai Walibya kuwa Ghadafi ndie anaeizuia Libya kupaa kimataifa na kwa kutumia walibya wachache wenye uchu wa madaraka wakaruhusu Gadafi kuuwawa na leo hii Libya iliyokuwa na huduma bora za kijamii kuliko Marekani imekuwa nchi ya kunuka mizoga ya binaadamu kila kona ya nchi yao. Kwa kweli watanzania tujifunze kuwa na shukrani kwa neema ile Mungu aliotujaalia kwani Mungu ametuhimiza hivyo na tusipofanya hivyo Ghadhabu zake huwa ni kali Mno. Kwa kifupi tu kamwe Marekani hawawezi kuwa na bifu na raia wa nchi husika kwa ajili ya Maslahi ya nchi husika siku zote inakuwa kwa ajili ya Maslahi ya nchi yao ni hii ndio Sera ya Marekani.Hata kama kutakuwa na watanzania wamejipelekesha kutumika kumsaliti Makonda na Tanzania ukweli utabaki pale pale Marekani huangalia maslahi ya nchi yao kwanza. Mfano mmoja tu ni ule uhusiano mzuri kati ya serikali ya China na Mkuu wa Mkowa wa Daresalaam,halafu wewe mwenyewe utapata jawabu kwani kiuhalisia Daresalam ndio Tanzania.
    Tukirudi kwenye mada yetu ya Simba kupendelwa nadhani VAR ingetumika tu kwenye ligi kuu. Naona tayari timu kama Simba wapo kwenye level kubwa zaidi kulingana na uwezo wa marefa wetu tukubali hilo.simba wanaweza kucheza caf champions league wakafika nane bora wakati marefa wetu hawawezi kuaminiwa na caf kuchezaesha hata mechi za awali na hapo ndipo utajua tatizo lipo wapi.

    ReplyDelete
  6. Kama goli la Kagere dhidi ya Coastal Union. Ni goli halali kabisa. Husikii kelele za VAR ya Yanga au kelele za waandishi uchwara waliopofuka kwa kupenda. Goli la kwanza la Yanga dhidi ya Prisons kabla ya penalti inayoweza kujadiliwa, Mapinduzi Balama alikuwa offside kabla ya kutoa pasi. Morrison aliye interfere pia alikuwa offside.Kelele zinapigwa??Hapana. Timu ina goal difference 31 inayofuata ina 14 Yanga wana 5 bado wavimba macho wanadai inapendelewa!!!

    ReplyDelete
  7. Enter your comment...Yana nilitaka kushangaa Saleh aache kuonesha mahaba yake kwa mikia ?

    ReplyDelete
  8. Ndio maana hatufiki mbali kimataifa, mizengwe imekua mingi

    ReplyDelete
  9. Jibu hoja. Wacha kisingizio cha kumlaumu Saleh Jembe amesema kweli au kasema uongo?Tujifunze kujibu hoja kwa hoja.Mimi ni Yanga lakini kwa hoja hii sina hoja ya kumpinga Saleh Jembe.Viongozi wa Yanga walituahidi ubingwa wameanza kutafuta visingizio.Tusijitoe kwenye reli tuukabili ukweli.

    ReplyDelete
  10. Naunga mkono hoja yako Saleh Jembe.Udhaifu ni wa marefarii wetu wa Tanzania ambao ni wachache sana wanachaguliwa kuchezesha za kimataifa.Inashangaza sana kulialia kuwa Simba inapendelewa wakati ni timu iliyoingia nane Bora ya klabu bingwa Africa...sijui walipendelewa na hao marefarii wa nje??? Bila soni wakaleta uzushi wa Simba kupulizia madawa vyumba bila kujua uongo huo unaharibu taswira ya soka la Tanzania.Kwa hili nawekemea vingozi wa Simba na TFF Kwa kutowachukulia hatua na hata kuwafungulia mashtaka walio chanzo cha kuwapakazia Simba ilifanya hujuma hizo kwa timu pinzani.Povu ruksa lkn matusi hapana ni hoja Tu.

    ReplyDelete
  11. Hapo leo umesema la mana Sana kwa kuutendea wema mpira na uzidi kuwaelemesha hao wanaofikiria kuwa kwa njia hiyo ndio itayowapa ubingwa ambao wameshavunjika moyo kuupata

    ReplyDelete
  12. Tatizo njaa, baada ya kuitetea Azam bila mafanikio umeamua kuhamia simba uone kama Mo atakuona. Haya maoni mbona sikuyaona wakati Yanga ikiwa chini ya Manji? Kelele za upande wa pili zilikuwa hizihizi! Na kwanini uwatuhumu viongozi wakati kila baada ya tukio Azam wanapost na kuuliza umeona nini hapa? Kama shida ni takwimu, nilitegemea uje na takwimu za Simba wamepewa penalt ngapi na magoli mangapi ya offside na Yanga na Azam wamepewa mangapi!! Hii ipo na si Bongo tu, hata EPL kuna wakati Arsenal ilikuwa inaongoza kutoa penalt tena wakiwa hm na Man U wakiongoza kupewa penalt katika uwanja wao wa nyumbani. Salehe unaongozwa na roho, kama wewe ni msema kweli mara ngapi umelizungumzia au kulifanyia kazi swala la rushwa michezoni? Kama wewe ni mtenda haki umeshazungumza nini kuhusu kitendo cha Wawa kumkanyaga Nchimbi kwa makusudi? Ukweli uko palepale kuwa utashangiliwa na uliowatetea ila haibadilishi maana kuwa soka la bongo limetawaliwa na rushwa. Kwahiyo usitumie kigezo cha waamuzi kukosea mechi moja ama mbili kuhalalisha kitendo cha waamuzi kufanya yaleyale kwa timu ileile katika mechi zaidi ya saba. Kabla ya kuwatuhumu watu, fanya utafiti kwanza. Nilitegemea uje na takwimu ili ubishani uwe kwenye takwimu na sio kuandika blabala ili kuhalalisha uozo. Ndio maana niliacha kusoma gazeti lenu la championi baada ya kugundua mnaandika mapenzi yenu badala ya uhalisia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic