MCHEZO wa leo wa Ligi Kuu Bara kati ya JKT Tanzania dhidi ya Coastal Union uliopaswa uchezwe kwenye Uwanja wa Isahmuyo majira ya saa 10:00 sasa ni rasmi utachezwa Uwanja wa Uhuru.
Ofisa Habari wa JKT Tanzania, Jamila Mutabazi amesema kuwa sababu kubwa ya mchezo huo kuhamishiwa Uwanja wa Uhuru ni maji kujaa kwenye Uwanja wa Isahmuyo.
"Tulipaswa tucheze kwenye Uwanja wa Ishmuyo ila kwa sasa hautachezeka tena kutokana na maji kujaa eneo la kuchezea, tumeamua kuupeleka Uwanja wa Uhuru, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema.
JKT Tanzania mechezo wake wa mwisho ilichapwa bao 1-0na Polisi Tanzania pia Coastal Union nao walichapwa mabao 2-0 mbele ya Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment