ODION Ighalo, mshambuliaji mpya wa Manchester United amesema kuwa alikubali kupunguzwa mshahara ili atimize ndoto yake ya kucheza ndani ya Old Trafford.
Ighalo, aliyewahi kuichezea Watford amesema kuwa hakulala wakati anasubiri kusaini mkataba na timu yake mpya, amejiunga kwa mkopo United akitokea Klabu ya Shanghai Shenhua hadi mwisho wa msimu huu.
"Wakala wangu alinipigia simu saa tano usiku, nilipopata dili hilo niliamka fasta na kutafuta mkalimali ili tuweke mambo sawa na nilimwambia wakala wangu afanye dili hilo bila kujali kama nitapunguziwa mshahara," amesema.
Raia huyo wa Nigeria mwenye miaka 30 amesema kuwa mama yake alilia kwa furaha aliposkia dili la mwanae kutua United.
0 COMMENTS:
Post a Comment