February 6, 2020


Mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula hajakaa langoni kwenye klabu hiyo tangu alipodaka katika mchezo wa ligi wa Simba dhidi ya Yanga, Januari 4, 2020.

Katika mchezo huo, Manula alilalamikiwa na mashabiki wa Simba hasa katika bao la pili alilofungwa na kupelekea mchezo kuisha kwa sare ya maba0 2-2, huku Yanga wakiibuka mashujaa kwa kutoka nyuma kufungwa mabao hadi mchezo kumalizika kwa sare.

Tangu mchezo huo, imepita jumla ya michezo tisa, Aishi Manula hajaanza golini na nafasi yake ikichukuliwa na mlango Beno Kakolanya.

Baada ya mchezo wa Simba na Yanga, timu ilielekea visiwani Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi ambako ilicheza mechi tatu na Beno Kakolanya alicheza katika michezo miwili huku Aishi Manula akiwa hajakaa langoni katika mchezo wowote.

Michuano ya Mapinduzi ilipomalizika na Simba kufungwa katika fainali na Mtibwa Sugar, timu ilirejea bara kuendelea na ratiba ya ligi na Kombe la Shirikisho, ambapo katika mechi sita mfululizo mpaka sasa Simba haijamuanzisha Manula katika mechi zote na badala yake Beno Kakolanya akianza katika michezo mitano ya ligi na mchezo mmoja wa Kombe la Shirikisho.

Ni wazi hilo ni suala linalomuumiza Manula kwani inahatarisha nafasi yake katika kikosi cha Simba pamoja na timu ya taifa, ikizingatiwa kuwa yeye ndiye golikipa namba moja wa Taifa Stars kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic