
NA SALEH ALLY
WAPENDA soka lazima watakwenda Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakiwa na mambo mengi kichwani tayari kuishuhudia mechi ya watani wa jadi Yanga watakaokuwa wenyeji wakiwakaribisha Simba keshokutwa Jumapili.
Bila shaka itakuwa mechi nyingine ambayo inajitegemea kama ambavyo zimekuwa mechi nyingi za watani wa jadi wanapokutana.
Haiwezi kufanana na mechi nyingine kwa kuwa kila mechi ya watani inakuwa na sababu zake za kupatikana au kufanyika.
Katika mechi ya keshokutwa, Yanga watakwenda uwanjani kikubwa zaidi wanakitaka ni heshima na kidogo kujaribu kuikamata Simba, jambo ambalo kiuhalisia linaweza kuwa na wepesi tu kama Simba watakuwa si makini katika mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Bara.
Ndio maana nikasema, Yanga watataka heshima lakini pili ni kuthibitisha kwamba ile sare ya mabao 2-2 baada ya tambo nyingi za Simba, kwao haikuwa ya kubahatisha.
Hayo ni mawazo ya tambo za soka lakini hebu tujadili kuhusiana na hizi ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa kila unapofikia mchezo wa watani wa jadi.
Umesikia wewe mwenyewe kuwa klabu moja imewaahidi wachezaji wake kiasi fulani cha fedha kama wakiifunga Yanga au Yanga wakiifunga Simba.
Viongozi wanalazimika kuweka dau mezani ili wachezaji wacheze vizuri na kuhakikisha wanapata ushindi, binafsi naona ni jambo la kufedhehesha mpira wenyewe na hili linatubakiza nyuma sana sisi katika mchezo wa soka.
Wachezaji wanaijua kazi yao, wanatambua wajibu wa kuifunga Simba au Yanga na wanajua umuhimu wa ushindi ndio maana hufanya mazoezi kwa juhudi kubwa, husikiliza maelekezo ya mwalimu kwa usikivu wa juu ili kuhakikisha wanafanikisha ushindi.
Juhudi zao pamoja na kujua watapata pointi tatu ambazo ni muhimu lakini wanajua namna inavyokuwa heshima kushinda dhidi ya mtani wao kwa kuwa mashabiki ambao huwaunga mkono wanahitaji ushindi huo kwa nguvu zote na lazima kuwafurahisha.
Angalia, wakati unawafurahisha watu unaotegemea wakuunge mkono, wakati huohuo unapata pointi zako muhimu ambazo zinaifanya kazi yako kuwa imetukuka. Sasa kuna haja gani ya kuongezewa dau la fedha ili uifanye kazi yako kwa ufasaha?
Binafsi huwa sioni ni jambo sahihi na wakati mwingine tunapaswa kwenda na wakati na kujifunza kutengeneza wachezaji wanaojitambua kwa kuwaacha wafanye kazi yao kwa weledi na viongozi wafanye yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawalipa fedha zao kwa maana ya posho na mishahara kwa wakati.
Tunaweza tukawa tunaona jambo hili ni dogo kwa kuwa tu ushabiki umewazidi wengi nguvu lakini hili jambo ni ugonjwa mkubwa sana ambao huenda tiba yake inaweza ikachukua muda mrefu sana kupatikana.
Wachezaji wanapaswa kulipwa vizuri na kupata kila kinachostahili ili wafanye vizuri. Wakati mwingine klabu zinalazimika kuwa watumwa kwa kuomba fedha kwa wafadhili ambao wakati mwingine nao wanakuwa na masharti yao baadaye, jambo ambalo si sawa.
Klabu zinalazimika kuwa watumwa kwa kuwa zinahitaji fedha za “kuwanunua” wachezaji wake ili waweze kuifanya kazi yao vizuri ya kumfunga mtani kwa kuwa kama watapoteza viongozi watakuwa katika wakati mgumu na hawaitaki hiyo presha.
Mikataba ya wachezaji na klabu haionyeshi hilo kwamba lazima wapewe fedha ndio wacheze vizuri dhidi ya Yanga au Simba. Kuendelea hivi ni kuendelea kutengeneza furaha ya kipindi hiki tu lakini uhalisia, tunatengeneza bomu kwa muda mrefu sana na kuna siku litakuwa tatizo kubwa ambalo kulimaliza kutahitaji nguvu nyingi sana.
Mfano, klabu imeahidi Sh milioni 150 kwa wachezaji waifunge Yanga au Simba, kwa nini fedha hizo zisingetumika kutengeneza uwanja au kuwakuza vijana kwa kuwanunulia vifaa sahihi wachezaji wa vijana au ziwe mishahara au posho za wachezaji wa timu za vijana na wanawake kwa muda wa miezi mitatu, minne kuliko iishe siku moja kwa kuwalipa wale ambao walishalipwa kwa mujibu wa mkataba!
Nawakumbusha, tuliache hili kwa kuwa kuendelea kulifanya ni kufanya mambo ya leo tu bila ya kuangalia kesho ya mpira itakuwaje.








Kwanza kabisa hongera kwa hili,isipokua nikuweke wazi tu YANGA HAWEZI KUMKAMATA SIMBA TENA NA UKITAKA KUAMIN HILI NJOO TAIFA KESHOKUTWA,kama umekaa unajidanganya nakudanganya uma pole sana kwa hilo,na pia nikwambie kitu ndugu simba sio timu yakuahidi wachezaji hela,simba wamejitosheleza kila idara wanalipwa vizuri,makazi safi na kila kitu,walimu wamekaa nakuwasoma wachezaji wanataka nini kwa muda mrefu na ndiomana wanafanya mambo makubwa kila kukicha,hivyo ningekushauri kama mjumbe ndani ya klabu yako pendwa ya yanga nenda ukawashauri acha kuzunguka nakutafuna maneno hapa.
ReplyDeleteAkawashauri kufanya mageuzi ya uendeshaji wa klabu. Hii ya kupewa ahadi kwa kuwafunga wapinzani then baada ya siku tatu unafungwa na timu nyingine kutokana na uchovu wa kukaza katika mechi ya dabi hakuna maana.
DeleteAkawashauri kufanya mageuzi ya uendeshaji wa klabu. Hii ya kupewa ahadi kwa kuwafunga wapinzani then baada ya siku tatu unafungwa na timu nyingine kutokana na uchovu wa kukaza katika mechi ya dabi hakuna maana.
DeleteKWANI ALIYEAHIDI MILIONI 200 NI NANI??
ReplyDeleteKwahyo kwa akili yako unategemea simbabatafungwa mechi 6 na yanga atashinda mechi zake zote alizobaki nazo?maana hapo ndio atakua amemkaribia simba.
ReplyDeleteTAKWIMU YANGA POINTS 47 MECHI ZILIZOBAKI 14 MPE ZOTE INAMAANA ATAPATA 42,THEN JUMLISHA ATAKUA NA 89 SIMBA ANA POINTS 68 NA ANA MECHI 12 MPE MECHI 7 TU NYINGINE ZOTE APIGWE INAMAANA ATAKUA NA 89 BADO YANGA ANA KIBARUACHA MAGOLI HIZO NDIZO TAKWIMU JIPANGE SANA MTANI KIBARUA SIO KIDOGO USHINDE MECHI ZOTE 14 ALAFU SIMBA APIGWE MECHI SITA HA HA HA HA HA SIJUI KAMA NI KAZI RAHISI.
ReplyDeleteKwani tunaposema motisha tunamaanisha nini? Ile ni kama motisha tu kwa wachezaji, hata kwenye ajira zingine tunaona namna watendaji wanavyopewa motisha inaleta hamasa, ufanisi na umakini katika kutekeleza majukumu yao. Na hiyo motisha inatolewa na wadhamini wao wala hawakulazimishwa. Kwangu sijaona tatizo hapo na makala kama hizi nadhani hazileti afya katika michezo yetu. Nadhan ungetumia muda wako kuandika makala nyingine si kubeza na kuona motisha iliyotolewa na watu wenye mapenzi na timu yao si lolote si chochote. Kwanza hata nyumbani mtu anapomwambia mwanangu ukifanya vizuri kwenye jambo fulani nitakupa zawadi hiyo nayo haifai? Nayo imepitwa na wakati? Kwani utafiti wako umekupa majibu kuwa huko walikoendelea hawatolewi ahadi katika mechi kama hizi?
ReplyDeleteWhy motivation is conducted only during kariakoo derby?dont you see that is dangerous?anyway lets wait and see,ila sijawahi ona aina hii ya ujinga tangu nizaliwe kwa mara ya kwanza naushuhudia Tanzania klabun yanga,ina sumu inajengeka vile mtu atakua hajitumi mpaka akiona motivation kwa table ndio ana struggle as slave to win the victory,and despite of these are the real factors that hinders the positive development of African football,dont do these purposely.
DeleteHivi hujui kuwa kila Yanga ikishinda inapewa motisha? Hapa motisha imeongezwa tu lakin inatolewa katika kila mchezo toka GSM ianze kuidhamin Yanga
DeleteWasijitie tamaa wala wasijidanganye. Mpira Mara nyingi ni mchezo wa bshatinasibu. Wanaweza kuifunga Simba kama ilivo tokea kwa Mwadui kukishinda Simba kwa goli moja na Yanga kuchapwa tatu Bila na na Kagera, lakini kusema Yanga iifunge Simba na baadae Simba ifunguwe michezo Sita kama wanavoweseka waliorukwa na akili, ni juu yetu tuwaonee huruma kwakuwa wamezugwa kama wale wanaoutaka utajiri kwa viungo vya binaadamu. Masikini Roho zao wanautamani ubingwa Bila kujipima hali zao zilivyo
ReplyDeleteKwa hiyo ninyi mnapoweka kuponi za kujishindia gari au bodaboda kwenye magazeti ya championi mnakuwa mnaturudisha kati kama siyo nyuma?! So muandike vizuri tu kiueledi halafu muwaachie wananchi wachague gaxeti la kununua?
ReplyDeleteUkisoma kidogo performance management utakua umuhomu wa incentives....kama umewahi kufuga mbwa utajua ni kwa nini tunaweka masega ya nyigu kwenye chakula cha mbwa
Yanga ni mafala
ReplyDeletewataje kabisa kuwa YANGA ndio wametoa ahadi hyo
ReplyDelete