March 10, 2020


KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amesema kuwa anawaomba radhi mashabiki kwa kitendo chake cha kumchezea mchezo usio wa kiungwana kiungo wa timu ya Yanga, Fei Toto.

Wakati Simba ikichapwa bao 1-0 na Yanga, Chama alimchezea rafu Fei Toto ambayo mwamuzi hakuiona ispokuwa kamera za Azam TV zilinasa tukio hilo.

Chama amesema kuwa amemalizana na Fei Toto kwa kuwa alimuomba msamaha baada ya kumaliza mchezo huo na kuelewana hivyo anaomba msamaha kwa mashabiki.

"Najua nilifanya kitendo kisicho cha kiuungwana ila ilikuwa ni kitendo ambacho sikutarajia, nimemuomba msamaha Fei Toto na kwa sasa ninawaomba radhi mashabiki,".

2 COMMENTS:

  1. Sasa subiri kamati ya saa
    720 maana sio 72 iamue

    ReplyDelete
  2. The weak never forgives. Forgiveness is the attribute of the strong

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic