March 22, 2020


UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa umeamua kumuweka pembeni kwa muda Kocha Mkuu wa timu hiyo Felix Minziro ili kutibu majeraha yake ya mguu aliyoyapata.

Alliance FC ya Mwanza ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 29 za Ligi Kuu Bara.

Yusuph Budodi, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa Alliance amesema kuwa wameamua kumpa mapumziko Minziro.

"Tumeamua kumpa mapumziko Kocha Mkuu Minziro kutokana na kuumia mguu wa kulia alipopata ajali atakapokuwa vizuri atarejea kuendelea na kazi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic