March 22, 2020


UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa una mkataba mrefu na nyota wao Agrey Morris ambaye anakipiga ndani ya Azam FC.


Beki huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji.


Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria,amesema kuwa Azam FC walimuongezea mkataba beki huyo kutokana na ubora wake akiwa ndani ya uwanja.


 "Morris ni mchezaji wa Azam FC na mkataba wake aliongeza wakati akiwa Hospitali baada ya kuumia kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ila kuhusu kuibukia Simba hilo kwa sasa halipo, mashabiki wa Azam FC wasiwe na mashaka.


"Mchezaji mzuri anahusishwa kujiunga na timu kubwa kutokana na umuhimu wake hilo lipo wazi lakini ukweli ni kwamba hakuna mazungumzo yoyote ambayo tumeyafanya kwa sasa na Simba," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Acheni kuzusha wapumbavu nyie,mngetuonyesha au kututhibitishia wapi simba alitangaza kumtaka moris?ujinga uliokithiri huo acheni ujinga plz.

    ReplyDelete
  2. Kawaida yake huyu mwandishi kuwapandisha chati wachezaji kwa kutumia mgongo wa simba

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...yan Kama simba wanamtaka Morris asiseme,nyie mnaoitetea simba kwa nn,hao n waandishi ndo kazi yao na wanahaki ya kuzielezea team zooote ikiwemo simba kwan simba kitu gani,acheni izo na simba ndo wanaoongoza kunyemekea wachezaj wa team nyengine mbn bocco,nyoni na kapombe waliandika na ikawa kweli huo ni ushamba kuona simba ni club ambayo haina tetesi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic