March 9, 2020

Verified

BAADA ya Simba jana kuambulia kichapo cha bao 1-0 mbele ya Yanga Uongozi umewataka mashabiki kutulia na kukubali matokeo yaliyotokea.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram namna hii:-"Wanasimba wenzangu niwape salaam zangu fupi za kuwaomba kwanza tukubali tumepoteza mchezo wa jana kwa kufungwa na timu ilyocheza vizuri kuliko sie,na tukubali hilo halibadiliki kwa sasa,najua tumeumia ila hiyo ndio football tuliyoichagua kuipenda.

"Kwa tamaduni zetu lazima tucharurwe kama ambavyo tungewacharura iwapo tungeshinda,but life goes on(Maisha yanaendelea). Muhimu kujipanga kwa mchezo unaofuata keshokutwa,tusitoke ktk reli na sote tunajua ubingwa upo mikononi mwetu ,tusithubutu kumtafuta mchawi wala kulaumiana.

"Wametufunga kihalali kabisa na ni haki yao kutamba!!
But Insha'Allah tutachukua ubingwa wetu," .

13 COMMENTS:

  1. Leo Manara umeongea ambalo hujawahi kuliongea ktk usemaji wako wa club ya simba. Ukweli aliyeshinda alicheza vizuri kuliko aliyefungwa

    ReplyDelete
  2. Leo umeongea kimpira, sasa naanza kukuelewa

    ReplyDelete
  3. ITAKUA KAJIFUNDISHA SPAIN BAADA YA KUSHUHUDIA REAL MADRID IKILALA MBELE BETIS

    ReplyDelete
  4. Aje na mguu toka ulaya msemaji wao kama alivoahd

    ReplyDelete
  5. Aje na mguu toka ulaya msemaji wao kama alivoahd

    ReplyDelete
  6. Kuanzia sasa aache kabisa tambo zake dhidi ya Yanga.

    ReplyDelete
  7. Kufungwa sawa ila kama viongozi wa Simba wataendelea kutia pamba masikioni mwao na kusajili wachezaji wanavyopenda wao basi wanasimba tutaendelea kuteseka kwani tumepiga kelele tena na tena kwamba mabeki wa Simba mpaka kunako kiungo mkabaji kuna tatizo kubwa. Na mabeki wetu wa sasa wataonekana wazuri kunako mechi za kawaida tu lakini wanapokutana na washambuliaji matata kidogo ni shida tupu na ni majanga zaidi kama Simba itafanikiwa kucheza caf champions league.Na kwa kupitia mechi ya Yanga utaona kwa kiasi gani fowadi ya kagere Boko ilivyochoka na kushindwa kuwa na mbinu mbadala ya kulazimisha matokeo. Suala la kutafutwa fowadi asilia mwenye uwezo mzuri wa kufunga limekuwa kigugumizi Simba kwa muda mrefu sasa labda kwa matokeo ya mechi hii ya yanga viongozi watamka. Simba bila ya kuyafanyia marekebisho ya mapungufu kadhaa kwa baadhi ya wachezaji na kutafuta wachezaji wenye uwezo basi hata aje Guardiola atachemka tu. Kwa sasa wanasimba tunatakiwa kukaa chini na kutafakari ila kilichowapa Yanga jeuri ni ile mechi ya kwanza ya ligi na ni kutokana na udhaifu wa beki ya Simba ndiko kulikokuwa kunakowapa tambo za kujiamini na yanga wataendelea kujiamini mbele ya simba ikiwa Simba hawatafanyia marekebisho beki yake na nahisi Simba kuna rundo la mabeki wengi wasio na msaada wa kuwachalenji akina Nyoni na Wawa,kuna haja gani wa kuwa nao?

    ReplyDelete
  8. Ingawa wengi wanasema tuliachie benchi la ufundi lkn kama kuna madhaifu ni lazima wapigiwe kelele na wajitafakari.Ingawa kila kocha anakuja na falsa yake ya ufundishaji na aina ya wachezaji anao wataka lkn bado anapaswa kuwashikirisha kikamilifu wale alio wakuta benchi la ufundi.Nashindwa kuelewa ni kwa vipi wachezaji Ndemla, Mpilipili na Abdul Rashid wamekuwa hawaonekani kucheza hata angalau basi dk 15 za mchezo.Majibu anayo kocha na benchi lake la ufundi ingawa hawataki kutupa majibu.
    Yusuf Mlipili na Ndemla walikuwa wanacheza mechi kadhaa chini ya makocha Omog na Lichantre na Abdul Rashid chini ya Aussems alipata kucheza mechi kubwa kama ile dhidi ya VITA na alipeform vizuri lkn vipi siku hizi hawaonekani? ni majeruhi? hawaonyeshi viwango mazoezini? kocha anawabania?
    Mi nikiwa mdau wa Simba napata mashaka sana na wachezaji wetu tulio nao na tukifanikiwa kushiriki klabu bingwa ya Africa basi amini usiamini yatatukuta yale ya UD Songo.Wachezaji wetu wengi wako slow na hili limedhihirisha perfomance inayoonyeshwa ktk michezo ya ligi ya hapa nyumbani na kombe la FA.
    Kwa hakika haipingiki kuwa Simba itachukua ubingwa wa VPL TZA tena wa msimu huu lkn tunajiandaje kukabiliana na timu tutakozocheza nazo za klabu bingwa za Afrika? Tena mechi zenyewe zinaanza baada ya miezi minne na ushehee tokea sasa kwa maana ya mwezi wa August, 2020.Au tutaendelea kuimba taarabu zetu za kuwa hatukujiandaa vya kutosha, hatukuwa na bahati na tutajaribu next year?
    Ikiwa kweli tumedhamiria kuifanya timu ya Simba kuwa mshindani ktk michezo ya kimataifa basi bodi ya wakurugenzi inapaswa kuyavulia nguo maji na kuyaoga na kuacha mzahaa wa kubahatisha kuleta wachezaji ambao mwisho wa siku tunashuhudia madudu uwanjani.Inabidi bodi iingie sokoni na inunue wachezaji wa maana na si lazima kununua utitiri wa wachezaji.Binafsi naona ni wachezaji watatu/wanne tu wa uhakika wanao hitajika hata kama budget kwa hao wote itakuwa tzsh 1 to 1.5 bilion na kuachana kununua utiriri wa wachezaji kwa tzsh 30m...50m tena eti toka Brazil.Ukiangalia timu kubwa kama Ahli hutasikia wamenunua wachezaji zaidi ya 7 kwa msimu mmoja na hii ni kwa sababu wanaziba mapungufu na si kusajili kufurahisha mashabiki ambao mwisho wa siku tunaishia kuwazomea hawo hawo wachezaji waliosajiliwa na mifano ipo.
    Kwa kumalizia tumeona game zetu mbili dhidi na Yanga na madhaifu ni yaleyale ya mabeki wa kati, kiungo mkabaji aliye na nguvu, na washambuliaji wepesi asilia wa kati ni muhimu sana.Na udhaifu huu huu ulikuwepo hata mechi ya majuzi ya Azam.

    ReplyDelete
  9. Mimi ni Simba kindakindami, lakini ushindi wa kibao kimoja walichokipata umenifurahisha Sana kwakuwa baada ya miaka ya kuchapwa na droo kidogo nao wametabasamu na kupata nguvu za kuikebehi Simba na huku muungwana Mooakiqapa hongera jambo ambalo Hawa jamaa hawajawahi kulifanya hata moja isipokuwa kulalamika na kebehi. Jamaa waliishi kwa unyonge muda mrefu na si kitu kutoshukuru au kuendelea na matusi huko mitaani kwasababu wamelewa kwa furaha na tusiwalaumu na tusijali kebehi, ao pale Mnyama atapokabidhiwa ubingwa wake. Sisi tutasherehekea ubingwa na wao goli lao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic