March 9, 2020

NYOTA wa zamani wa Barcelona, Cristian Tello ameipa nafasi timu yake ya zamani kubaki namba moja kwenye msimamo wa La Liga baada ya kuifungia bao la ushindi timu yake ya Real Betis wakati ikiichapa mabao 2-1 Real Madrid.

Bao la kwanza la Real Betis lilifungwa na Sidnei dk ya 40 na likasawazishwa na Karim Benzema dk ya 45+3 kwa mkwaju wa penalti na lile la ushindi lilifungwa na Cristian Tello dk 82.

Ushindi huo unaifanya Real Madrid kubaki na pointi zake 56 ikiwa nafasi ya pili na nafasi ya kwanza ipo kwa Barcelona yenye pointi 58 huku Real Betis ikiwa nafasi ya 12 na pointi 33.

Barcelona ilimtoa nyota huyo Kwa mkopo mwaka 2014 na baadaye waliamua kumuuza mazima nyota huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic