March 9, 2020



NAONA mashabiki kwa sasa wanajua kilichotokea jana Uwanja wa Taifa ambapo Yanga waliikaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba mchezo wa kwanza uliochezwa Januari 4, Uwanja wa Taifa timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 Jambo ambalo lilisababisha baadhi ya wachezaji wa Simba kubebeshwa zigo la lawama kutokana na matokeo hayo kwani wao walianza kufunga mabao mapema na yakapinduliwa na wapinzani wao Yanga.

Tumeona kwamba kiungo mzawa Mzamiru Yassin inaelezwa kuwa ni majeruhi na ukifuatilia hakuna anayeweka wazi ni nini kilimsumbua  zaidi ya danadana nyingi kupigwa juu yake.

Naona ni aina ya soka ambalo linaleta ukakasi na kila mmoja hajatambua hatma ya Yassin mpaka sasa atakaa benchi mpaka lini licha ya uwezo wake ambao ulianza kuonyesha matunda na kwa timu ya Taifa ya Tanzania.

Tuachane na hayo ya Yassin ambaye aliporwa mpira na Mapinduzi Balama aliyefunga bao kwenye mchezo huo uliochezwa Januari na kumuacha nyota huyo kwenye mzigo wa lawama.

Pia achana na matokeo ya jana ya Yanga kushinda bao 1-0 mbele ya Simba, kwani kila mtu tayari ameshajua ambacho kilishatokea kikubwa ni kuangalia yajayo kwenye maisha ya soka letu.

Pointi yangu hapa ninataka kusema kwamba suala la matokeo na lawama kwa wachezaji kisa kufungwa ni jambo ambalo linaua vipaji vyao na kuwapa maumivu ambayo hawastahili.

Rai yangu kwenye matokeo kila mmoja atambue kila mechi ina matokeo tofauti timu iliyojiandaa kushinda ndiyo inayoibuka na matokeo suala la kwenda na matokeo linawaponza wengi.

Tukiachana na hayo kwa sasa tunaona moto wa Ligi Daraja la Kwanza unazidi kukata mbunga na ushindani unazidi kushika kasi.

Naona kila timu inapambana kuibukia Ligi Kuu Bara ila zinasahau kuwa huku juu ushindani wake ni mkali pia wanapaswa wajiandae pia kwa hilo.

Kwa zile ambazo zitapata bahati ya kupanda kwenye ligi ni lazima zianze maandalizi kwa sasa kabla hazijapanda ili zisije kuangukia pua .

Timu nyingi ambazo zinapanda ligi huwa zinaweka juhudi kubwa kupanda na kusahau kwamba kuna umuhimu wa kuanza maandalizi mapema pia ya namna watakavyofanya ndani ya ligi. 

Mfano mzuri timu ya Namungo FC imeweza kufikia malengo yake kwa sasa na imekuwa ikipata matokeo mazuri sawa na Polisi Tanzania ambazo zote zilipanda msimu huu.

Licha ya kwamba zinafanya vizuri bado zina kazi ya kuona namna gani zitadumu kwenye ubora huo ndani ya msimu huu na ule ujao zisije zikatetereka. 

Tunaona kitu ambacho kipo kwa timu zetu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kuweka nguvu kubwa kupanda Daraja na kusahau kuna kushuka pia.

Rai yangu kwa timu zote kujipanga kufanya vema Daraja la Kwanza na kwenye Ligi pia ziweke nguvu ya kutosha na kufanya maandalizi sahihi huku chini itakayowapa misingi imara ya kudumu watakapofika juu.


5 COMMENTS:

  1. Work rate ya Muzamiru ni one of the best in the league. Kama hana injury ni makosa makubwa sana kumuweka nje ya uwanja. Hata kwa Ndemla kukosa game time ni makosa. Game zote tatu tulizofungwa 1-0 tuliishiwa mbinu ya kufikia lango kwa sababu hakuna wapigaji mashuti ya mbali.

    ReplyDelete
  2. Ndemla na huyo mzamiru atamuweka nan benchi !!kua makin simba ina professionals

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli Simba ina mapro wanaozidiana ila kiukweli hata huwezi kuwaanzisha hao hao kila mechi na hasa zinapokuwa nyingi. Lazima wote wacheze wasaidiane.

      Delete
  3. Mimi naona mwandishi wa hii makala kachanganya mada. Kichwa cha habari kikuubwa kinazungumzia Mzamiru Yasin kiungo wa Simba kutocheza kwa muda sasa tangia mechi ya kwanza ya Simba na Yanga ya sare ya 2 - 2. Taarifa zilizopo ni kwamba Mzamiru ni majeruhi lakini ameanza mazoezi kidogo kidogo. Kwenye pre-match meeting ya juzi ( Yanga na Simba) tulimsikia kocha wa Simba akisema kwamba kwasasa ana majeruhi wawili, Ndemla Said na Miraji Athumani "Sheva". Kwahiyo, huo ni ushahidi tosha kwamba Ndemla ni majeruhi na hawezi kucheza, wakati Mzamiru ndio kwanza anarejea toka kuwa majeruhi na asingeweza kucheza pambano hilo.

    Nimesema mwandishi anachanganya mada kwasababu kichwa cha habari kinamzungumzia Mzamiru ( nadhani ndio ile tabia ya waandishi wa magazeti ya michezo hapa nchini ambayo sasa imeota mizizi ya kujiandikia tu kichwa cha habari chenye mvuto kwa wasomaji lakini habari iliyopo ndani ni kichekesho kabisa, hakuna weledi, hakuna maadili wala misingi ya uandishi)lakini katikati ya habari anaondoka kwenye mada kuu anazungumzia maswala ya ligi kuu kwa juu juu hivi, kisha tena anaondoka hapo anazungumzia ligi daraja la kwanza ambayo ndio inahitimisha makala yake.

    Sasa tafakari msomaji mwenzangu aina hii ya uandishi wa habari....kwamba habari ya mchezaji Mzamiru Yasin imekwenda hadi ikageuka kuwa habari ya ligi daraja la kwanza. Kwa baadhi yetu Blog ya Saleh Jembe ni kama chai ya asubuhi tunaamkia hapa kusoma taarifa za michezo na nyinginezo duniani. Tunaheshimu makala za Saheh Jembe kutokana na kuandikwa kwa weledi na takwimu sahihi na za kutosha. Ushauri wangu kwa Saleh Jembe ni kwamba ahakikishe waandishi wa habari za michezo wanaotumia Blog hii wawe na weledi wa kutosha na taaluma ya kutosha kuweza kuandika taarifa sahihi na zinazoleta tija. Kwa lugha nyingine, waandishi wawe na vuwango vya Saleh jembe mwenyewe. Hii ndio Blog pekee inayotoa taarifa na makala za soka kwa mfumo bora, wa kisasa na wenye taarifa nyingi mpya. Ni Blog ya michezo ambayo inafanya updates nyingi mara kwa mara. Hivyo, wasomaji wengi tunapenda kupata habari habari hapa Saleh Jembe. Hivyo, tumwombe Saleh Jembe ajitahidi kuzingatia ubora wa Blog hii na asiwaache waandishi wenye uwezo mdogo wa kuchambua habari waharibu taswira ya Blog hii pendwa.

    NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  4. Ni kweli uandishi huu ni shida.Story zile za socks kuvuka kiatu kikabaki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic