March 20, 2020

BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji wa Yanga leo amerejesha mkataba wake kwa mabosi wake ambao ni kampuni ya GSM kupitia kwa Mkurugenzi wa uwekezaji Hersi Said baada ya kumalizana nao muda mrefu alipotua ndani ya Yanga.

Morrison alisaini dili hilo la miaka miwili mwezi Februari kabla ya mechi ya Machi 8 dhidi ya Simba Ila hakurudisha mkataba wake kwa mabosi wake.


Kwenye mechi hiyo, Morrison alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 44 lililoipa pointi tatu Yanga, Uwanja wa Taifa.

Hali hiyo imekuja kutokana na kuenea tetesi kwamba ameingia kwenye anga za Simba ambao walikuwa wanaiwinda saini yake

6 COMMENTS:

  1. Amesaini mkataba na GSM au na Yanga???Haya maigizo yatatuletea matatizo wanayanga. Kila mmoja asiye kiongozi akiamua kumsainisha mchezaji wake itakuwaje?Hamna mfungamano wa wachezaji kwani watakuwa na mabosi tofauti. Huu mkanganyiko upp hata sasa kwani kuna wachezaji wanalipwa na GSM na wengine hawalipiwi.

    ReplyDelete
  2. Mimi nilizani Yanga tumeshaachana na utaratibu huo mbovu wa usajili tumesahau huko nyuma uluvyoathiri timu? Kila tajiri na mchezaji wake siku tajiri haelewani na timu na mchezaji wake anadengua kuitumikia klabu. GSM tunawakubali wasaidie timu lakini wapitie kwa viongozi wetu halali tuliowachagua. Haya maonyesho ya kuonekana GSM ndio mmemsajili Morison hatuyataki hayana tija hata kwa wachezaji wengine wanajisikiaje? Hii ni timu ya wananchi sio timu ya GSM.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Brother umezungumza common sense.Welldone sana.Baadae itakuwa matatizo na lazima utokee msuguwano ili kuepuka huu ndio muda muafaka wa kurekebisha matatizo

      Delete
  3. Tumekuwa branch ya GSM. Tutavuna tunachopanda.

    ReplyDelete
  4. Tafuteni pesa ili mumsainishe nyie. Njaa tu, mnaropoka tu. Nyinyi ndio mliempinga manji badala yake alipoondoka mkakaa kimya, na njaa ikatawala yanga. Sasa mnaanza chokochoko na GSM. Embu tuachieni yanga yetu, anaetaka yoyote asajili. Kama nynyi mnaotoa comments pia tunawaruhusu mlete pesa za usajili, mmekalia majungu tu wakati hamna hata Kumi

    ReplyDelete
    Replies
    1. comments ni lazima lakin hata kilichozungumzwa ni cha muhimu na ni lazima kizungumzwe kwani wao hawazungumzwi kisa wana hela? ebo utumwa huo sasa hapa kuna makosa kuhalisia hivi leo GMS inasitisha mkataba kabla ya miaka miwili na akaja mdhamini mwingne huoni kutakuwa na shida? et hatuna kumi eheeee koma

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic