March 20, 2020


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba leo amerejea nchini Rwanda kwa ajili ya mapumziko mafupi baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kwa muda wa siku 30.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuirtia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilisimamisha mikusanyiko yote isiyo ya lazima ili kuzuia kuenea kwa Virusi vya Corona.

Kagere leo ameelekea Rwanda ambapo anatarajiwa kurejea baada ya Ligi kuanza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagra amesema kuwa:" Usalama kwanza na ni matumaini yangu kila kitu kitakuwa sawa bakini salama.

Wakati Ligi Kuu Bara inasimama Simba inaongoza ikiwa na pointi 71 na Kagere ni kinara wa kutupia akiwa na mabao 19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic