March 21, 2020

IBRAHIM Ajibu yupo kwenye majanga makubwa ndani ya Simba kwa kuhofia kushindwa kuvunja rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita alipokuwa ndani ya Yanga kwa kutoa pasi nyingi za mabao na kufunga pia.
Alipokuwa Yanga msimu wa 2018/19 Ajibu alikuwa namba kinara kwa kutengeneza pasi za mwisho ambapo alitoa pasi 17 na kufunga mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara huku bao lake la kubinuka mbele ya Mbao FC likiwa ni bao bora la msimu.
Mpaka sasa Ajibu akiwa ndani ya Simba inayoongoza ligi ikiwa imecheza mechi 28 ametengeneza pasi nne za mwisho za mabao na alifunga bao moja mbele ya Polisi Tanzania wakati Simba ikishinda mabao 2-1 Uwanja wa Taifa akiwa na deni la pasi 13 na mabao matano ili avunje rekodi yake.
Ajibu ambaye Yanga alikuwa anavaa kitambaa cha unahodha, amecheza mechi 16 kati ya 28 ambazo zimechezwa na Simba na alipotua Simba.
Ametumia dakika 705 uwanjani akiwa na wastani wa kutoa pasi baada ya dakika 176 ambapo alitoa pasi hizo kwa Miraj Athuman wakati Simba ikishinda mabao 2-0 mbele ya Biashara United, Sharaf Shiboub na Clatous Chama mbele ya Mbeya City na Jonas Mkude wakati Simba ikivaana na Mbao FC.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic