March 21, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo ilikuwa na matukio mengi ambayo aliyaona jambo alilokuwa akiwahurumia wachezaji wake kutokana na mazingira wanayopitia.

Kwenye mchezo uliochezwa Machi 15, Uwanja wa Majaliwa, Yanga ilikubali sare na kugawana pointi mojamoja mbele ya Namungo.

Kwenye mchezo huo Yanga ilianza kupata bao la kuongoza kipindi cha kwanza kupitia kwa Tariq Seif na lilisawazishwa na Bigirimana Blaise, kipindi cha pili.

Eymael amesema kuwa mazingira ambayo walipitia mpaka kufika Ruangwa hayakuwa rafiki jambo lililomfanya awaonee huruma wachezaji kutokana na kucheza wakiwa wamechoka.

"Safari yetu ilikuwa ngumu kutokana na umbali wa eneo pia ubovu wa barabara ulitufanya muda mwingi tuwe tunarushwarushwa ndani ya basi na tulifika tukiwa tumechoka, katika mazingira haya inakuwa ngumu kupata ushindi.

"Ninatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inapata ushindi hata wachezaji pia wanapambana kupata ushindi lakini wakati mwingine mazingira yanawakataa," amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo imecheza mechi 27 imejikusanyia pointi 51 kibindoni ikiwa imefunga mabao 31.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic