March 21, 2020

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa alikuwa anashangazwa na taarifa zilikuwa zikieleza kwamba yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa Simba ilihali anaitumikia Klabu ya Yanga.

Morrison raia wa Ghana amesajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo msimu huu na amekuwa na mchango ndani ya timu yake kwa kutimiza majukumu ndani ya uwanja.

Amefunga mabao matatu ndani ya Ligi Kuu Bara na ametoa pia pasi tatu za mabao wakati Yanga ikiwa imefunga mabao 31 kwenye mechi 27 ilizocheza.

Nyota huyo alikuwa akihusishwa kujiunga na watani wa jadi wa Yanga ambao ni Simba kutokana na kuvutiwa na uwezo wake ndani ya uwanja aliouonyesha kwa muda mfupi.

"Nilikuwa nashangazwa na habari kwamba ninajiunga na Simba ilihali nilikuwa naitumikia Yanga, ninachokijua mimi ni mali ya Yanga na nitaendelea kuitumikia Yanga.

"Kuhusu kutakiwa na Simba ni vitu ambavyo vipo ukizingatia mimi ni mchezaji hata nilipokuwa nje ya Tanzania kuna timu zilikuwa zinahitaji ila mwisho wa siku nikajiunga na Yanga.

"Nawapenda mashabiki wa Yanga wamekuwa wakionyesha tabia za kipekee kwa kujitokeza uwanjani na kufurahi pamoja nasi nami nitaendelea kupambana ndani ya Yanga," amesema.

Mkataba wa awali Morrison alikuwa amesaini miezi sita aliongeza mkataba mwingine ambao ni wa miaka miwili jambo lililowapoteza kwenye ramani wapinzani wao Simba.

1 COMMENTS:

  1. Habari za kutakiwa na Simba zilitengenezwa na nyinyi waandishi ili muuze magazeti

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic