March 21, 2020


SVEN Vandernbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wamechoka kutokana na kucheza mechi mfululizo jambo ambalo lilikuwa likimpa wakati mgumu kwenye kupanga kikosi na kuwapa mapumziko wachezaji wake.

Mwezi Machi, Simba ilicheza mechi nne ambazo ni sawa na dakika 360 na ilishinda mechi tatu na kuambulia kichapo mechi moja ilikuwa Machi 8 mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa.

Mechi zake nyingine ilikuwa mbele ya KMC, Machi Mosi ambapo ilishinda kwa mabao 2-0 Uwanja wa Uhuru, Machi 4, ilikuwa mbele ya Azam FC, iliposhinda kwa mabao 3-2 Uwanja wa Taifa na Machi 11 ilishinda mbele ya Singida United mabao 8-0.

Kufuatia agizo la Serikali kusimamisha mashindano yote yanayohusisha mijumuiko ya watu ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona, Sven amesema kuwa watatumia muda wa mapumziko kurejea kwenye ubora.

"Wachezaji walikuwa wananiambia kwamba hawapo fiti asilimia mia kutokana na kucheza mechi mfululizo kwa sasa watapata muda wa kupumzika na kurejea kwenye ubora wao.

"Ninaamini itakuwa bora kwetu na nafuu kwani itawafanya wacheze kwa umakini kuufukuzia ubingwa ambao tunautaka kwa sasa, nilikuwa natumia nguvu kuwapa mapumziko mafupi jambo ambalo lilikuwa likiwafanya wapumzike muda mfupi" amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza imecheza mechi 28 kibindoni ina pointi 71.

3 COMMENTS:

  1. Una wachezaji wengi lakini unang'ang'ania walewale

    ReplyDelete
  2. yaani watanzania sijui tupoje akibadilisha kikosi mnalalamika akipanga wale wale mnasema anarudia wachezaji mhhh

    ReplyDelete
  3. kila timu ina first eleven, na hii ni michuano mikubwa tena ya ligi unadhani combination inaundwaje akibadilisha kila leo? tuweni watulivu kocha akiwa anafanya maamuzi yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic