March 23, 2020


IMEELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mpango wa kumrejesha kundini mshambuliaji wao wa zamani Obrey Chirwa anayekipiga ndani ya Azam FC.

Chirwa kwa sasa ni kinara wa kutupia ndani ya Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba akiwa amefunga mabao nane sawa na David Molinga wa Yanga.

Wakati wa usajili wa dirisha kubwa msimu huu, Chirwa alikoswakoswa na Yanga kutokana na Kocha wa wakati huo Mwinyi Zahera kugoma kumpokea kutokana na kile alichoeleza kuwa ni mchezaji anayependa fedha.


Yanga ikiwa imecheza mechi 27 ambazo ni sawa na dakika 2,430 imefunga mabao 31 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 78.

3 COMMENTS:

  1. Yanga,Yanga,Yanga kelele ndio mafanikio yao ndani ya miaka mitatu mfululizo Simba akichukua ubingwa.Sijawai kuona timu ikifirahia kufeli kama Yanga. Waandishi nao wanapiga hela kwa kutumia jina la Yanga lakini Yanga yenyewe hata huyo mfadhili wao hajaekwa hadharani wanaifadhili yanga kwa mikataba gani? Azam ndio mpinzani halisi wa Simba kihali na mali hata kwenye mbio za ubingwa na hapo ndipo utakapofahamu kuwa Yanga inapambwa kwa sifa za kijinga kwani Yanga inaweza kusajili mchezaji akawa anaitia ufukara timu kwa gharama na akawa kazi yake ni kufanya mazoezi na kulala akisubiri ligi pasi ya kushiriki mechi za kimataifa kama si ujinga kitu gani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. wakati Yanga wakichukua ubingwa mara tatu mfululizo hukuyasema haya
      sasa zamu yenu imekua nongwa !!
      hawa matajiri hawachelewi kuondoka Yanga walikua na Shirazi, Virani, Gulamali na Manji ambao leo hawapo hivyo mnavyotamba mbakishe na akiba

      Delete
    2. Nyie si mmenunuliwa sasa basi mtuache sisi tuhangaike kelele za nini?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic