LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wanachoka kwa kucheza mechi nyingi mfululizo jambo ambalo analifanya ni kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake ili kuwapa muda wa kupumzisha akili kabla ya kuvaana na Simba, kesho, Machi 8,2020.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakicheza bila kupata muda wa mapumziko tangu usiku mwaka 2019 ambapo Desemba 24 walicheza na Mbeya City na kulazimisha suluhu.
“Tumekuwa na ratiba ngumu ambayo inabana tangu X-Mass, tulikuwa tunacheza na mechi zetu nyingi ni ngumu, kazi ninayofanya kwa sasa ni kuwapumzisha baadhi ya wachezaji ili wapate nafasi ya kupumzika,” amesema.
Wachezaji ambao wamekuwa wakipumzishwa mara kwa mara na Eymael ni pamoja na Mrisho Ngassa, Papy Tshishimbi, Mohamed Issa, Yikpe Granimien.
Malalamiko hayana balance. Simba mechi zake zilikuwa kama hizo lakini hatujasikia malalamiko
ReplyDeleteHao yanga kwel wanazingua kila kukicha wanalalamika awaeleweki tatizo nn
ReplyDeleteHivi ninyi mikia mwahitaji mtu asemeje muelewe!!? Hapo amesema hatochezesha wachezaji wote au katika mipango yake ameona apumzishe wengine!!? Jitambuen sio mnaandika comment ziczo na weredi wa kusoma kinachomaanishwa.
ReplyDelete