March 21, 2020


WALLACE Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni wanaotumika ndani ya Tanzania iwapo wataondoka nchini hawataruhusiwa kurudi tena nchini kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Corona.

Karia amesema kuwa, Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari kwa ajili ya Virusi vya Corona hivyo wanaondoka na kwenda nje ya nchi huko hawatambui aina ya maambukiza yapo kwa kiasi gani.

"Hawajapewa likizo wachezaji bali ligi imesimama kwa ajili ya tahadhari ambayo inachukuliwa kwa sasa, kwa wachezaji wa kigeni watakaokwenda kwenye nchi zao katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama, hawataruhusiwa kushiriki ligi ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

"Tutawasiliana na mamlaka husika ili kuona namna gani tutawazuia na hawataweza kushiriki kwenye ligi iwapo hali itatulia kwani tahadhari kuchukuliwa ni muda wote na sio muda mfupi," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Leo karia amegeuka serikali wakati watalii hawajazuiwa yeye anazuia wachezaji

    ReplyDelete
  2. Upuuzi muongo mkubwa güni watalii wamejaa tele humu

    ReplyDelete
  3. Aende zake huko akazuie mipaka kila siku ndege zinashusha watu kuliko wachezaji wa hapa AFRIKA MASHARIKI, muongo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic