KOMBE la Shirikisho limezidi kupamba moto na kwa sasa tayari timu nane zimetinga hatua ya robo fainali ambazo ni Simba, Yanga, Azam FC, Ndanda , Sahare All Stars, Kagera Sugar, Alliance na Namungo ila balaa lilikuwa kubwa kwa timu za Ligi Kuu kupata tabu mbele ya zile za Ligi Daraja la Kwanza.
Simba iliyo chini ya Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji aliponea chupuchupu kukwama Stand baada ya kushindwa kuulinda ushindi wake alioupata dakika ya 51 kupitia kwa Hassan Dilunga na kuipa nafasi Stand United kusawazisha dakika ya 67 kupitia kwa Miraj Saleh.
Ilitinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa penalti 3-2 zilizojazwa kimiani na Clatous Chama, Deo Kanda na Hassan Dilunga ila Meddie Kagere na Ibrahim Ajibu walikumbwa na bundi la kukosa penalti, Uwanja wa Kambarage.
Azam FC mabingwa watetezi walishikwa shati na Ihefu FC ya Mbeya inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa kutoshana nguvu ndani ya dakika tisini na kushinda kwa penalti 5-4 Uwanja wa Soloine, Mbeya.
Yanga Uwanja wa Uhuru, iliokolewa na Haruna Niyonzima aliyefunga bao la ushindi dakika ya 45 na kuizuia Gwambina inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kuleta madhara licha ya ushindi huo Gwambina walionyesha ukomavu, Uwanja wa Uhuru.
Ndanda FC wao waliibamiza Kitoyasa mabao 3-1 na kujikatia tiketi ya kushiriki robo fainali, Kagera Sugar ilishinda kwa penalti 2-0, Uwanja wa Kaitaba, Baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90 huku JKT Tanzania ilitolewa na Alliance kwa mikwaju ya penalti 5-3 baada ya dakika tisini kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1
Mbeya City ilitolewa na Namungo kwa kufungwa mabao 2-1 ikiwa Uwanja wa Sokoine, kwenye timu nane zilizotinga hatua ya robo fainali ni timu moja tu ya Ligi Daraja la Kwanza ambayo ni Sahare All Star ilipenya baada ya kuifunga mabao 5-2Panama Uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment