March 20, 2020

NADIR Haroub, Meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amewataka wachezaji kuendelea kufanya mazoezi kipindi hiki cha mapumziko ya dharula kwa ajili ya kujikinga na kusambaa kwa virusi vya Corona.

Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili, Ligi ya Wanawake, Ligi ya Mabingwa wa Mkoa, Umitashumta na shughuli zote za kimichezo zimesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja na Serikali kutokana na kupambana na kusambaa kwa Virusi vya Corona.

Haroub amesema :"Kipindi hiki cha mapumziko kwa wachezaji ambayo ni maalumu kwa ajili ya kupambana na kusambaa kwa Corona ni lazima wachezaji kujilinda afya zao na kufuata kanuni za afya, wasisahau pia kufanya mazoezi.

"Ni muhimu kwa wachezaji kufanya mazoezi kwani ndio asili yao iwapo watashindwa kufanya hivyo itawarudisha nyuma kwenye uwezo wao," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic