March 7, 2020


KESHO Machi 8 2020, Uwanja wa Taifa,Simba itakuwa ugenini ikicheza mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.
Simba ipo chini ya Mbelgiji Sven Vandenbroeck huku Yanga ikiwa chini ya Luc Eymael ambaye naye pia ni raia wa Ublgiji.
Rekodi zinaonyesha kuwa msimu wa mwaka 2014/15 kwenye mchezo wa watani wa jadi uliochezwa Machi 8 mabingwa watetezi walikuwa nyumabani na waliikaribisha Yanga.
Simba ilishinda mchezo huo kwa bao 1-0 lililofungwa na Emannuel Okwi dakika ya 52
Kesho saa 1:00 Yanga itakuwa nyumbani ikiikaribisha Simba na itakuwa Machi 8 swali kubwa litajibiwa kesho ambapo kila timu imejipanga kupata ushindi.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa msimu huu Simba ikiwa mwenyeji ilishuhudia Yanga ikipindua meza kibabe na kuufanya ubao kusoma 2-2.

Simba ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao moja lililofungwa na Medie Kagere na kipindi cha pili waliongeza bao la pili kupitia kwa Deo Kanda.

Kwa upande wa Yanga meza ilipinduliwa na Mapinduzi Balama pamoja na Mohamed Issa.

2 COMMENTS:

  1. Umeandika ty ilimradi simba aonekane nae ana makelele kama yanga,sasa huyo Okwi anahusika nn tena hapo?waongelee akina kagere na kanda unaonekana wazi kabisa kwamba unaforce ili uonekane kwamba umeandika habari za simba pole sana ila tambua kwamba simba ni timu inayojielewa katika nyanja zote yani usije ukakaa ukafikiria kwamba simba wataropoka kama ndugu zako yanga futa kabisa hilo wazo,usilazimishe uongo kuuweka kwenye gazeti utaaribu kazi yako.

    ReplyDelete
  2. Sasa umeandika nini we bibi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic