May 21, 2020


ATUPELE Green, mshambuliaji wa Bashara United amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya kuona ligi ikirejea kutokana na maandalizi ambayo anayafanya.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona kuna dalili za kurejea hivi karibuni kutokana na Serikali kusema kuwa hali inazidi kuwa shwari.

Atupele amesema:"Mimi nipo fiti kwa kuwa ninafanya mazoezi kulingana na maelekezo ambayo nimepewa na mwalimu hivyo sina mashaka iwapo ligi itarejea hivi karibuni kwani nimeukumbuka sana mpira,".

 Biashara United ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 29.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic