May 5, 2020


OFISA Habari wa Klabu ya simba, Haji Manara amefunguka kuwa anakosa amani kila anapowaza janga la Virusi vya Corona kwa kuwa hajui litakwisha lini.

Manara alisema anajiuliza kama itawezekana tena dunia kurudi katika hali yake ya kawaida na watu kuendelea na shughuli zao kama ilivyokuwa awali bila kuwa na hofu zaidi, huku akisema anahisi kuna kitu ambacho Mungu anatufundisha kupitia janga hili.

Manara aliweka sauti kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alisikika akisema: “Mimi najiuliza, hivi tutarudi siku moja kama dunia kuwa katika hali ya kawaida, yaani tukaishi kama zamani, harusi, sherehe, hitima zikasomwa na kuwekeana sinia za ubwabwa.

“Tutarudi na watu tukaaminiana na hakutakuwa na kukwepana, watu wataingia misikitini na makanisani kufanya ibada bila hofu, mimi mwenzenu nina hofu sana, nimejawa na nyingi hofu sioni kama kutakuwa na namna ya watu kushirikina tena kama awali.

“Walimwengu mimi nina hofu sana, siku ya tatu hii najiuliza hili swali, hamuoni kama kuna jambo Mwenyezi Mungu anataka kutufundisha kitu kupita kwa haya maradhi aliyotuletea?

“Najua sayansi itakataa ila mimi naamini ipo sababu ya Mungu katika jambo hili, siujui mtihani ulioikumba dunia nzima kwa wakati mmoja kuliko huu, tufanye jitihada zetu za kibinadamu lakini kimbilio kuu iwe Mungu Mwenyezi,” alisema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic